Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama, akimtangaza mwimbaji kinara wa Tamasha la Krismasi 2013 kutoka Afrika Kusini, Pastor Solly Mahlangu “Obrigado” ambaye ataimba na kundi lake uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Desemba 25.
===== ===== ====
WAKATI Tamasha la Krismas likikaribia, muimbaji nguli wa muziki wa Injili wa Afrika Kusini, Solly Mahlangu ‘Obrigado’ni mmoja wa waimbaji ambaye anatarajia kuimba kwenye tamasha hilo linalotarajia kuanza Desemba 25 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama mwimbaji huyo ataimba live siku hiyo pamoja na waimbaji wake wengine 14.Msama alisema mwimbaji huyo anatarajia kushiriki katika tamasha hilo jijini Dar es Salaam, tamasha ambalo litafanyika pia katika mikoa ya Morogoro (26), Tanga (28), Arush(29) na Dodoma (1).
Aidha Msama alisema bado wanaendelea kufanya mazungumzo na waimbaji wengine yameshakamilika kwa waimbaji wa ndani na nje ya Tanzania ikiwa ni pamoja, Solomon Mukubwa (Kenya), Ephraim Sekeleti (Zambia), Liliane Kabaganza (Rwanda). Waimbaji wa Tanzania ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Edson Mwasabwite, New Life Band na John Lissu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...