Familia ya Bwana Martin Mpankuli
wanapenda kukupa maendeleo ya shughuli za msiba wa mke wake Maua
Mpankuli,(pichani)
Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuondoka
Leeds pamoja na Mume wa Marehemu leo tarehe 7 Novemba 2013 kuelekea Dar Es
Salaam, Tanzania. Mwili wa marehemu utawasili Dar Es Salaam siku ya Ijumaa
tarehe 8 Novemba 2013 saa Tisa mchana (15:00).
Kwa wale waliopo Tanzania, shughuli
za msiba zitafanyika nyumbani kwa Kaka wa mume wa marehemu Bwana G E Maganga,
Kijitonyama- Kwa Ali Maua. Mazishi yanatajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe
9 Novemba 2013 makaburi ya Kinondoni, Dar Es Salaam.
Kwa mawasiliano zaidi kuhusu shughuli
za msiba Dar Es Salaam, wasiliana na:
Mr Edga Maganga – 0755 454544
Mrs Happy Rwechungura – 0754 607710



Lala salama dada Mauatutakukumbuka daima.tunaamini umekwenda mahala pazuri dada Mwenyezi Mungu ni mwema na mwenye rehema
ReplyDeleteLala kwa amani dada Maua our super sister