MKONGWE
wa muziki wa dansi Kassim Mapili amethibisha kushiriki Tamasha la Gurumo 53
litakalofanyika Jumamosi ya tarehe 14 mwezi Desemba mwaka huu.
Mapili
amesema si yeye tu, bali pia ataratibu mpango mzima wa kuhakikisha wakongwe
wote wa muziki wa dansi wanashiriki tamasha hilo bure bila malipo yoyote.
Tamasha
hilo ambalo ni mahsusi kwa ajili ya kumuaga mwimbaji mkongwe Muhidi Maalim
Gurumo litafanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe.
Mratibu
wa tamasha hilo, Juma Mbizo amesema Mapili ameamua kubeba jukumu la kuandaa
wakongwe ambao ambao watatengeneza wimbo maalum wa kumuaga Gurumo utakaosikika
kwa mara ya kwanza TCC Club Disemba 14.
Baadhi
ya wakongwe wengine waliothibitsha
kushiriki Tamasha la Gurumo 53 ni pamoja Komandoo Hamza Kalala, Tshimanga
Kalala Assossa na Waziri Ali.
Gurumo
anaagwa kufuatia kutangaza kwake
kuachana rasmi na muziki wa jukwaani baada ya kudumu kwenye kazi hiyo kwa miaka
53.
Bendi
za Twanga Pepeta, Msondo Ngoma na wanamuziki kibao waliowahi kung’ara na Sikinde
ni sehemu ya wasanii watakaosindikiza tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu.
Hadi
kustaafu kwake Gurumo aliyezitumikia pia bendi za Kilimanjaro Chacha,Rufiji
Jazz, Kilwa Jazz, Sikinde na OSS – Ndekule, alikuwa ni kiongozi na mmoja wa
wamiliki wa Msondo Ngoma.
Wasanii
waliowahi kuitumikia Sikinde ambao watakuwepo kumsindikiza Gurumo ni pamoja na
Cosmas Chidumule, Abdallah Gama, Hussein Jumbe, Mashaka Shaaban, Kalamazoo,
Henry Mkanyia na Karama Legesu. Wengine ni Ali Yahaya na Boniface Kachale,
Benno Villa Anton, na Ibrahim Mwinchande.
Hata
hivyo, licha ya wasanii hao waliowahi kuitumikia Sikinde kuwemo kwenye tamasha
hilo, bendi ya Mlimani Park “Sikinde Ngoma ya Ukae” haitashirki katika Gurumo
53 kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wao.
Mbizo
amesema Mlimani Park ina mkataba unaowabana kufanya onyesho lolote
litakalowakutanisha na Msondo hadi baada ya sikukuu ya Krismasi (Disemba 25,
2013).
Juma
Mbizo amesema licha ya Sikinde kutoshiriki tamasha hilo lakini nyimbo zote
zilizotamba ndani ya bendi hiyo ambazo zilitungwa na Gurumo, zitarindima TCC
Club kwa ubora ule ule.
“Wanamuziki
wengi waliofanya kazi na Gurumo katika Sikinde enzi hizo, hawako tena katika
bendi hiyo, hivyo watakuwa huru kuungana na mwimbaji huyo mkongwe na kushusha
burudani nzito.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...