Habari zimetujia sasa hivi zinasema abiria kadhaa akiwemo Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli  Mh Edward Lowassa wamenusurika kifo, baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuwa pasuka matairi yote manne ya nyuma wakati ilipokuwa ikitua katika uwanja wa Arusha leo mchana. 
Ndege hiyo ya shirika la ndege la precision aina ya ATR ilipata ajali hiyo wakati ikitua, ambapo Matairi yote manne ya nyuma yalipasuka na kusababisha taharuki kubwa kwa abiria. Ila hakuna mtu aliyedhurika katika ajali hiyo. 
"Yaani Mungu ni mkubwa kwa kweli, ametunusuru maisha yetu na kiongozi kipenzi chetu Lowassa...Mungu atamlinda jamani...siamini" alisikika akisema mama mmoja miongoni mwa abiria hao wakati akishuka.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Jamani sokoine alipata ajali mwaka 1984 na sio 1994. wenye data shukeni hapa

    ReplyDelete
  2. Hayati Sokoine alifariki 1984 na sio 1994.

    ReplyDelete
  3. Poleni kwa ajari! Mwenyezi Mungu anawalinda.

    Lakini Sokoine hakufariki mwaka 1994??? kama ulivyowasilisha.

    ReplyDelete
  4. Ahsante mungu kwa kuweza kuwanusuru watanzania wenzetu pamoja na raisi wangu mtarajiwa Mh.Lowassa

    ReplyDelete
  5. Hii ilikuwa iwe ajali mbaya sana kuwahi kutokea, lakini tunamshukuru MUNGU aliyewanusuru ndugu zetu hawa.

    Na pia siyo jambo la kawaida sana kutokea yaani tairi zote kupasuka kwa wakati mmoja.....hii ilikuwa hatari kubwa!

    ReplyDelete
  6. Rais wa wapigaji

    ReplyDelete
  7. Rais wa wapigaji

    ReplyDelete
  8. Poleni sana mlionusurika. Ni vizuri Lowassa the next president kushuhudia hayo kwani ataimarisha sekta ya usafiri wa anga atakapoingia madarakani.

    ReplyDelete
  9. Inshallah, Tunamshukuru sana Mola kwa kuepusha kifo kwa ndugu zetu hawa na kutoka wazima katika ajali hii.

    Tunawapendeni nyote. Hatupendi kuona hata Mtanzania mmoja anapoteza maisha kienyeji tu.

    ReplyDelete
  10. Pole sana mheshimiwa Lo. ndio ukubwa ndugu yangu, yote ni mipango ya Mungu. Ila jamani punguzeni ushabiki wenu mpaka katika hali kama hii mmekomaa tu 'prezidaa" "prezidaa". tuko wengi tunaowania kiti hicho: Ala!!

    ReplyDelete
  11. Safety regulation is not performing there duty

    ReplyDelete
  12. Nani alikuwa command in charge(Rubani) wa ndege hii?.Huyu naye anastahili pongezi zake.

    David V

    ReplyDelete
  13. Wakaguwaji wa ndege airpoti ,kitengo cha safety ya mamlaka ya aanga wanahusika kutowajibika

    ReplyDelete
  14. Mimi ni CCM damu lakini Lowasa simtaki kabisa na SIO Rais wangu.

    Hana Sifa ata chembe za kuwa Rais na ili ni somo kwa wanaccm wenzangu na Taifa lote, Labda awe rais wa wapigaji kama alivyosema mdau hapo juu maana nchi hii ina marais wengi ata Dimond na Madee ni marais pia!

    Abakie kuwa mfanyabiashara na mpigaji tu, Urais awachie wengine.

    ReplyDelete
  15. Mara nyingi nimesafiri na Precision air kwenda Arusha ninachoweza kusema nimekuwa ninikishuhudia HARD LANDING kutokana na uwanja kuwa mfupi hivyo marubani hulazimika kushuka kwa haraka ili aweze kutua mwanzo mwa njia ya kuruka na kutua Ndege.

    ReplyDelete
  16. Glory be to Almighty God

    ReplyDelete
  17. Duh,kuna haja ya kubadilika,kinachozungumzka ni ajali,masuala ya urais yanatoka wapi?
    Kuwa rais au kutokuwa rais si maamuz yako au yake bali ni mchakato na maamuz ya wa tz.

    ReplyDelete
  18. yaani hata kwenye mambo muhimu tunaweka ushabiki! sasa mtu anaripoti tukio hatari kama hili anakimbilia kudai sijui 'kiongozi kipenzi chetu' hizo siasa za urais 2015 zinakujaje hapa?!!

    ReplyDelete
  19. Pole jembe.

    ReplyDelete
  20. Hard landings may cause deflation to the tires any time.It is not an isolated issue as it is often happening in aviation. Congratulations to the crew for managing to control the situation.

    ReplyDelete
  21. Ni kweli ajali ni mbaya,lakini ajali kama hii ni ajali ambayo haitakiwi kuleta madhara makubwa kwani ni moja ya ajali ambazo marubani huambiwa,kufundishwa na kufanya mazoezi(simulation training) kwa hiyo rubani makini hujua la kufanya.Anaesema hii ni ajali kubwa sana haijawahi kutokea,I believe s/he is not serious.Goggle aircraft accidents and incidents you will understand what I mean.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...