Waziri wa Afya wa Zanzibar Juma Duni Haji na Naibu Mkurugenzi Mambo ya Afya kutoka jimbo la Changzhou Dk. Chen Jiangua wakitia saini makubaliano ya ujenzi wa kituo cha maradhi ya Mifupa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani na magonjwa ya tumbo Hospitali Kuu ya Mnazimmoja katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya wa Zanzibar Juma Duni Haji akibadilishana hati ya makubaliano na Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Afya wa Jimbo la Changzhou baada ya kutiliana saini makubaliano ya ujenzi wa kituo cha maradhi ya mifupa Hospitali ya Abdalla Mzee na Kituo cha magonjwa ya tumbo Hospitali kuu ya Mnazimmoja katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Muhammed Dahoma akiukaribisha ujumbe wa Madktari kutoka Jimbo la Changzhou katika sherehe za utiaji saini makubaliano ya ujenzi wa kituo cha maradhi ya mifupa na magonjwa ya tumbo katika Hospitali ya Abdalla Mzee, Mkoani Pemba na Hospitali Kuu ya Mnazimmoja katika sherehe zilizofanyika leo Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
Picha ya pamoja ya viongozi wa Wizara ya Afya ya Zanzibar wakiongozwa na Waziri wa Afya Juma Duni Haji na Ujumbe wa madaktari kutoka Jimbo la Changzhou ulioongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Afya wa Jimbo hilo baada ya kutiliana saina makubaliano ya ujenzi wa kituo cha maradhi ya mifupa Hospitali ya Abdalla Mzee na kituo cha maradhi ya matumbo Hospitali ya Mnazimmoja. Sherehe hiyo ilifanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...