Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe amefungua mkutano wa kwanza wa aina yake wa kupanga mapango mkakati wa utekelezaji , utunzaji na ulindaji wa vyanzo vya Maji pamoja na mabadiliko ya tabia ya nnchi Mjini Morogoro leo asubuhi.
Akifungua mkutano huo, Waziri wa Maji Prof. Maghembe aliwaomba wataalamu wa sekta mabalimbali kuandaa mpango huo ili Serikali sasa ianze kutekeleza mikakati yoye iliyopo ili kulinda vyanzo maji Nnchini.
’’ Ndugu zangu wote mnaelewa kuwa kwa sasa tatizo la uharibifu wa vyanzo vya maji ni kubwa kwa sababu ya uvamizi wa vyanzo vya maji,ukataji wa miti ovyo pamoja na uvamizi wa makundi makubwa ya mifugo katika vyanzo vya maji pamoja na ongezeko la upungufu wa ubora wa maji nnchini “ alisema Prof. Maghembe.
Alisema kuwa, anamini wataalumu watukuja na mpango ambao utalisadiia Taifa letu kukabiliana na balaa hili la Kitaifa. “ Kimsingi tuna sera ya maji, sheria ya Maji namaba 11 ya mwaka 2009 pamoja na mikakati mbalimbali hivyo ni wajibu wetu sasa kuhakikisha kuwa yale tuliojipangia tunayatekeleza “ alisistiza.
Waziri Maghembe aliwashauri wajumbe kuona uwezakano wa bodi zetu za mabode ya Maji kwa kushirikiana na wadau wengine kuanzisha ulinzi shirikishi katika vyanzo ya maji ili wananchi wawe walinzi wa raslimali hiyo.
Akimkaribisha Waziri waMaji, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr. Joel Bendera aliishukuru Wizara ya Maji kwa kuuleta mkutano huu katika Mkoa wa Morogoro kwani Mkoa wake ni Mkoa wa mfano maana kwa muda mfupi tangu awe Mkuu wa Mkoa wamefanikiwa mengi katika suala la utunzaji wa mazingira ikiwa pamoja na kukifunga kiwanda ch nguo cha 21st Century kilchokuwa kinatumia magogo ya miti tani 50 kwa siku pamoja na kutiririsha maji machafu katika mto Ngerengere. Alimfahamisha Prof. Maghembe kuwa Mkoa wa Morogoro una mito 143 na kwa mwaka karibu mito 133 hutiririsha maji mwaka mzima.
Mkutano huu unajumuisha watalaamu wa Uhandisi, uhandisi mazinngira, wachumi, maendeleo ya ya jaimii, wanasheria toka Wizara mbalimbali pamoja na asasi zisizo za kiraia.
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe akifungua mkutano wa Mpango mkakati wa utekelezaji wa kulinda na kuviendeleza vyanzo vya Maji pamoja na mabadiliko ya tabia yannchi Mjini Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr. Joel Bendera akimkaribisha Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe katika mkutano wa Mpango Makakati wa utekelezaji wa utunzaji wa vyanzo vya Maji.
Wadau na Wataalam wakisiliza kwa makini hotuba ya Mhe.Waziri Maji Prof.Jumanne Maghembe.
huyu mtu kila siku ni makongamano.acha maneno fanya kazi.hapo wamekula tayar bahasha zile la khaki.
ReplyDeleteNamuona mama Nsanya. Mwenyezi Mungu aendelee kumtunza na kumbariki daima.
ReplyDelete