Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel John Nchimbi(kushoto) akisoma Kibao cha uzinduzi rasmi wa Magereza "Duty Free Shop" ya Butimba, Mwanza ambayo itahudumia Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa(kulia) ni Kamishna Jenearali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel John Nchimbi(suti nyeusi) akifurahia jambo na Mmoja wa Wafungwa( kushoto) wa Gereza Kuu Butimba, Mwanza ambaye ni fundi Ushonaji wa nguo za aina mbalimbali mara baada ya uzinduzi rasmi wa Kiwanda cha Ushonaji cha Gereza Kuu Butimba. Kiwanda hicho kitakuwa kinatoa huduma ya Ushonaji wa Sare za Maafisa, Askari, Watumishi raia, Wafungwa pamoja na nguo za aina mbalimbali za Taasisi za Serikali na Watu Binafsi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa( kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel John Nchimbi( suti nyeusi) akiangalia nguo za aina mbalimbali kama ambavyo zinaoonekana katika picha ambazo zimeshonwa na Wafungwa katika Kiwanda cha Gereza Kuu Butimba, Mwanza ambapo Kiwanda hicho kimezinduliwa rasmi leo Disemba 02, 2013(kushoto kwa Dkt. Nchimbi) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja.
Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza toka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel John Nchimbi( hayupo pichani) ya uzinduzi rasmi wa Kiwanda cha Ushonaji cha Gereza Kuu Butimba, Mwanza pamoja na Magereza "Duty Free Shop"ya Kanda ya Ziwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel John Nchimbi(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza mara baada ya kuzindua rasmi Magereza "Duty Free Shop " ya Kanda ya Ziwa iliyopo Gereza Kuu Ukonga leo Disemba 02, 2013(kulia kwa Dkt. Nchimbi) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kushoto kwa Dkt. Nchimbi) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga(wa pili kulia) ni Rais wa Kampuni ya Transit Military Shop Limited, Bw. Sadrudin Virji( wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mwanza, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Magereza, Raphael Molel( Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...