PAMOJA NA BAADHI YA VIONGOZI WA MAJIMBO NA HII NI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 
  1. Kikao kilichofanyika ofisi ya Mkoa Ujiji kilibeba AGENDA ya Kujadili na Kuboresha ujio wa ziara ya Katibu Mkuu (T) Dr. P. Slaa Mkoani Kigoma 5/12/2013
 
-      Ambapo atatembelea majimbo yote 8 ya mkoa Kigoma kwa mikutano si chini ya miwili kwa kila jimbo na baadae mkutano wa mwisho, jioni Mkutano ufanyike makao Makuu ya Jimbo. Lengo likiwa kuangalia uhai wa chama.
 
-      Mambo makuu na muhimu yalizingatiwa
 
-      Usalama kwa Kiongozi huyo kufutia sakata la Maamuzi ya kamati kuu dhidi ya Mhe.Zitto na mapokeo ya wanachama wetu.
 
-      Kutoa taarifa rasmi kwa majimbo na kupokea hali ilivyo au inavyoonekana katika maeneo yao.
 
-      Baada ya Tafakuri ya kina na ya Hekima na Busara pevu katika ujio huo iliazimiwa ifuatavyo
 
i.             Mkoa uliomba Taifa lihairishe na kusogeza mbele tarehe ya ziara hiyo muhimu kwa mkoa wetu, ili Mkoa kama ngazi ya chini ya Kanda na Taifa uwezekwenda katika majimbo hayo na kuwaelimisha wanachama na wapenzi wetu juu ya kuheshimu na kuwa na nidhamu na maamuzi yatolewayo na ngazi ya juu yetu. 

Hata kama yanamaumivu ….katiba yetu ifuatwe katika kutatua tatizo – Maoni ya Wengi Mkoani na Viongozi wa Chama ni kuudhiwa na maamuzi ya k/kuu ambayo dhahiri yalilenga kumilika Zitto – Kisiasa.
 
ii.            Mkoa ulitishika na vitisho baada ya kupokea taarifa toka kwa baadhi ya viongozi wa majimbo ya mkoa kwa hali ya usalama si nzuri kwa ujio wa kiongozi wetu Dr. Slaa kufika Kigoma kwa kipindi hiki wakati wanachama na wapenzi wakitafakari na kwa kauli tofauti zisizolenga kuwepo usalama.
 
iii.           Kwa hekima ya kikao kilijiridhisha kwa kupata maoni toka katika majimbo 6 kuwa hali ni mbaya kabisa wakishauri Katibu mkuu asogeze mbele ziara yake kupisha mtafaruku huu na kwa usalama wa Chadema na viongozi wake Kitaifa.
 
iv.          Hivyo Mkoa kupitia kikao hicho kuwa ni bora kuzuia kuliko kutibu, tayari sintofahamu zimeonekana, viongozi na hasa wa majimbo kutofautiana mitazamo ni HATARI katika hali hiyo. Mkoa ulijiridhisha usalama hautakuwepo kwa ujumla hata kama baadhi ya majimbo yakisema wao wapo salama tu.
 
v.            HOFU/TAHADHARI -   Endapo hali haitokuwa salama Mungu apishe mbali.

Mkoa hautokwepa lawama na Uzembe wa makusudi kwani wajibu wa ngazi ya chini ni kutoa ushauri kwa ngazi ya juu. Hivyo mkoa unatoa ushauri kwa Makao Makuu (T) Chadema kusogeza mbele ziara hiyo hadi hali itulie na mkoa upite majimboni kujiridhisha na usalama kwa viongozi wake na hasa wa Taifa.
   
LENGO KUU:   NI KUHAKIKISHA CHADEMA TUNAPITA SALAMA KATIKA WAKATI HUU MGUMU KWETU – CHADEMA
 
Asanteni
  
                                               
ALHAJ. JAFARI KASISIKO                                           MSAFIRI WAMALWA
M/KITI MKOA                        01/DEC.2013                KATIBU MKOA
0756439200                                                                0786448443
0714439200                                                               0756448442
 
  
CHADEMA MKOA KIGOMA
 
 
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kigoma wamewastahi sana. Hata kuwajibu hivyo ni staha tuu..jamaa wale na mtu wao hapata kalika pale..amani ya chadema na viongozi wake wa juu kwenda Kigoma ita happen pale tuu kwa viongozi kurejea maamuzi na hukumu zidi Mh.Kabwe. ..rejeeni mezani msawazishe hii. .kwani imepinda na haitanyooka kamwe pale kigoma kama hamtanyoosha. ..kukomaa na ishu na msimamo wenu dhidi ya zitto ni majanga kwenye chama..Slaa kwenda Kigoma alhali anajua kunatension sijui anawajua wakigoma vizuri au bado wote mna zile idea za wote wa kigoma ni ma brother K..msijidanganye mkoa hatari sana ule..na unawatu wenye busara sana. .wanaojua sana siasa..na wanaijua sana nchi yao.Mimi naipenda Chadema ila kwa hili la Kabwe tumepishana kabisa hapo na amani tuendelee kuomba iwepo kwani mpaka sasa naona Volcano inakaribia kulipuka
    Mdau.

    ReplyDelete
  2. Hao wanaotishia amani kama ushaidi upo kwanini wasichukuliwe hatua? Naamini watu wa usalama wapo na ziara iendelee kama kawaida, wakati wa miungu watu umekwisha sasa!

    ReplyDelete
  3. hao wanaosema Kigoma hakuna amani nawaona ni mazumbukuku tu,huyo ZZK inamana yupo juu ya sheraia??acheni uchizi wenu.
    hata angekua ni mfalme tungemwajibisha tu endapo anavunja kanuni na taratibu za chama.na huko ndiko kuleta mageuzi ya kweli an cyo kumfanya zzk kuwa mungu mtu.
    kama ninyi wa kigome huyo ndie mungu wenu basi awe kwenu na mfungue chama chenye kutowawajibisha watendaji wake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...