TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa (pichani) ataanza ziara ya siku 20 katika mikoa ya Shinyanga na Kigoma, kuanzia Desemba 4-23, mwaka huu.
Lengo la ziara hiyo ambayo imetokana na maombi ya muda mrefu ya viongozi wa chama katika maeneo husika, ni kuimarisha na kukagua uhai wa chama katika majimbo ya mikoa hiyo.
Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakutana na wananchi katika mikutano ya hadhara ambapo atazungumzia masuala ya kitaifa na eneo husika, kisha atafanya vikao vya ndani na viongozi pamoja na wanachama.
Siku ya Jumatano Desemba 4, mwaka huu Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakuwa Wilaya ya Kahama, siku inayofuata Desemba 5, atakuwa Wilaya ya Kakonko, Jimbo la Buyungu na Desemba 6, atakuwa Jimbo la Muhambwe.
Ratiba ya siku zinazofuata itaendelea kutolewa kwa vyombo vya habari.
Imetolewa leo Jumanne, Desemba 3, 2013, Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari CHADEMA
mbona inasemekana bundi wa ffu katua juu la paa la fk.Slaa
ReplyDeletemmasai huyu anatafuta balaa huko kiigomaa kwa kabwe
ReplyDeleteje huko atazindua miradi ya maendeleo au anapeleka matusi
ReplyDeleteHapa duniani tunapita tuuuuuuuuuuuuu! watu wanaumana tu . Siasa za namna hii zitatupeleka kusiko.
ReplyDeleteHuko anaenda kuzindua miradi ya kuimarisha chama
ReplyDelete