Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Nafikiri ni kitu cha ajabu sana kwa kutoa picha za majengo ya vikwangua anga kama vinavyoitwa.Hii inchi yetu inapenda sana kuwa kama inchi zingine hasa zilizokwisha endelea lakini kuna mambo mengisana tena sana ya kuweza kurekebishwa na itachukua miaka mingi sana ili kufika hapa wenzetu waliondelea walipo.Inchi inakazana kujenga majengo mengi ya ghorofa yanayobana na mengi ninahuhakika yapo kwenye hatari ya kuja kuanguka siku za mbele.Kwa nini tunakazana sana na vikwangua anga wakati MAJI,UMEME WA BEI YA JUU naBARABARA na BEI CHAFU na HOSPITALI,SHULE kutojengwa kwa wingi na kuimarishwa na kuwapatia raia wake maisha bora ila tuko mbio kukazana kujenga vikwangua anga ambapo inaonekana ndio maendeleo.Tunashidwa kuwa na maji ya uhakika na umeme ambapo nchi nchi ziko mbion kwenye mambo mengine ya maana na sio maji na umeme.Tumekazana kuleta investors wa kuendeleza vikwangua anga eti kisa mji au jiji la tanzanai linakuwa la kisasa uku umeme na maji na huduma zingine nyingi ni za ajabu.

    ReplyDelete
  2. Kumebanana, kuchafu na kuna giza tororo. Huo mji bado sana....Mdau hapo juu kaeleza ukweli hakuna barabara, maji, umeme wa shida( unakatika katika ovyo na bei pia ipo juu sana kushinda nchi tajiri) Hapo bado sana michuzi ndugu yangu bado hakuwaki, linganisha na hapo tu Nairobi utaona tofauti.

    ReplyDelete
  3. ukienda kwenye hivyo vikwangua anga, maji hakuna, vyoo vinanuka yaani shida. Let's start with basics like mdau hapo juu mentioned.

    ReplyDelete
  4. New York nini!

    ReplyDelete
  5. Si mbaya lakini "Fly overs" ziko wapi?Msongamano wa Magari ni balaa Daresalaam na kuna joto hatari(humidity-high) December hii.Wenye magari yasiyo na viyoyozi watakubaliana na mimi kwamba fallen+joto=s%*%.Na haya majengo marefu kwa nini yasijengwe pembeni mwa jiji?

    David V

    ReplyDelete
  6. Hivi nyie mafala mnaojiita wa ughaibuni hamna kizuri cha Tanzania cha kusifia???vyote huwa mnaponda tu.watu wa ajabu sana nyie.wapumbavu sana.

    ReplyDelete
  7. Mdau uliyeanza na 'Hivi nyie maf..." nakuunga mkono kwani hayo wanayosema mengine ni ya uongo.

    Mumekwenda kwenye kikwangua anga gani cha kisasa mukaona hakuna maji au hata umeme ukikatika si generator linafanya kazi?

    ReplyDelete
  8. Mtanzania akishatoka nje ya TZ, basi ndo utamsikia TZ kunanuka, hakuna maji, n.k Huo ni upumbavu uliokithiri. Hakuna mtu mwenye akili akakashifu kwao.

    Kama unaona kwenu kuna kasoro basi ni bora ukasaidia kurekebisha angalau 0.0001%

    ReplyDelete
  9. nafurahishwa na ukuwaji wa nchi yetu na jiji letu la Dar. madhari inabadilika ila nakubaliana na wadau wengine kwamba mahitaji ya muhimu kama maji, umeme, usafi wa mji, n.k yapewe vipaumbele.

    Nami napenda kuongeze ya kwamba vikwangua anga vijengwe kwa uimara wa hali ya juu ili vidumu kwa mamia ya miaka bila kuporomoka na kusababisha maafa.

    Pia ningefurahi sana hiyo kasi ya ujenzi wa vikwangua anga ingeenda sambamba na kasi za kuwekwa taa za barabarani walau kwenye kila barabara yenye lami nchini.Hili huwa linanikera sana na nina amini linachangia ajali usiku, na ujambazi, maana mitaa na barabara zina giza totoroo.

    Halafu mitaro yote iwe anafunikwa, ili mtu , baiskeli, magari, n.k visiweze dumbukia huko mchana au hata usiku (hasa ukizingatia kwamba usiku ni giza).

    Jamani wahusika msikubali kukabidhiwa barabara ambayo mitaro haijafunikwa.

    ReplyDelete
  10. Mara nyingi wanaoponda ni wale ambao hata bongo ya sasa hawaijui pia yeye huku Tanzania hana hata kiwanja,sio nyumba,huko aliko analala kwenye chumba ukubwa wa korido,kazi anayofanya ni kusafisha vyoo vya watu au kulea vikongwe nk, basi anajiona bora kuliko watanzania wote. Huo ni utumwa.
    Tanzania is ours, tushiriki kuijenga na sio kuoponda.tumethubutu na jitihada zinaonekana so tusiwavunje moyo wanaojituma.
    Mkataa kwao ni mtumwa.

    ReplyDelete
  11. Hivi hao wanaotukana wanayo akili timamu? badala ya kushinda kwa hoja mnatukana, inaonekana hamjastaarabika. Wadau wameeleza ukweli kwamba hakuna maji, umeme wa uhakika, taa za barabarani, hakuna barabara, kumebanana, na mji hauna mpangilio ndiyo maana kila mara kunatokea majanga ya kuanguka hivyo mnavyoviita vikwangua anga. Mkubali kukosolewa, mmoja wenu hapo juu anasema msaidie kama mnaona hakuko safi, tutasaidia vipi wakati kuna mamlaka husika ambazo hatupaswi kuingilia....Acheni mambo ya kijamaa eti msaidie. Kusaidia kwetu ni kutoa mawazo hayo ambayo wengi wenu wanatutukana ovyo. Sijui mtakuwa lini...kuosha midomo tu.

    ReplyDelete
  12. Hakuna mtu anaeweza kuinvest billions of shillings akajenga gorofa lake kubwa bila ya kuwa na uhakika wa maji,umeme nk.
    Hiyo picha ya michuzi hapo juu vinawaka vibatari au??
    michuzi anatuonyesha jinsi gani nchi yetu inapiga hatua and how proud he is of his own lovely country.
    Tatizo wengi mnaona watanzania hawana akili mpaka kujenga majengo mabovu.ingekuwa hiyo picha imepigwa nchi nyingine hawa jamaa wangesifia kweli.
    Shame on them. Endelea kutuonyesha mazuri mengine zaidi michizi.wasituvunje nguvu hawa watumwa.tujenge nchi yetu na wakiamua kurudi tunawatumikisha na huku.

    ReplyDelete
  13. Kuna maelfu na malaki ya watanzania walioko nje ya nchi wanaofanya kazi wa bidii, na waliosoma vya kutosha katika vyuo vinavyoeleweka sidhani wewe anon hapo juu unaweza kuwatumikisha...usidharau watu ukaita watumwa hata siku moja, hao wanafanya kazi kama wanavyofanya kazi watanzania wengine huko nyumbani ila wewE unaona tatizo watu waki-comment mawazo yao bila ya kutukana, ni lini mtajifunza ustaarabu wa kuacha maneno machafu? Kwani lazima utukane usipokubaliana na mwenzio? Mbona huwa inawauma sana mkisikia watu wanatoa mawazo yao wakiwa nje ya nchi? Kuweni wastaarabu!

    ReplyDelete
  14. Dahhh mimi nimefurahishwa sana na wote mlioamua kuwaeleza ukweli hawa jamaa huwa wanatukera watu wengi sana maana hawana kizuri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...