Habari Kaka Michuzi, 
Swali langu ni fupi tu, Hivi unapotuma kajimzigo chako kutoka ulaya kisichokuwa na thamani yoyote Main destination ni Zanzibar lakini unaambiwa uende ukagomboe mwenyewe JNU Airport ni maana yake nini?

Mara ya tatu natuma kwa njia ya UPS courier mzigo unafikia Dar es Salaam agent wa UPS anakwambia ukitaka mzigo ukomboe mwenyewe safiri uje Dar es Salaam ulipe Document hand-over fees Tsh.55,000/ uende mwenyewe Airport au 

Lipa Tsh.90,000/- ya agent wa UPS na hatujui Malipo ya TRA na vile vile hatujui muda gani inaweza kuchukua mwezi au miwili 

Mzigo wangu tokea tarehe 12 December umewasili Dar es Salaam hadi hii leo haujapatiwa ufumbuzi na kumbuka hii ni DOOR TO DOOR service SIO DOOR TO AIRPOT 
Ndani ya mzigo kuna 

Audio Mixer ambayo haina thamani yoyote clearance ya kazini tu nimeona niitume Tennis table bat 1 na mipira ya mazoezi (£10.00 nimenunua ebay)  

jumla mzigo hata thamani ya £100 haufiki lakini imeshakuwa big deal 
sasa je kama huu mzigo unaenda ZANZIBAR kwani ni usifanyiwe Clearance ZNZ wakati pia ipo TRA kule? hadi mtu aende Dar es Salaam hivi hii ni haki?

Na hizi fee za hawa UPS hii ni haki mbona unapo book mzigo huambiwi kama utahitaji kulipa fee ya agent au ya kupewa document?

Wenye data naomba ufafanuzi au opinion zaidi nimeshalalamika UPS UK na wao wanasema wanasubiri info kutoka TZ kila nikiwapigia hapa Ila hadi hii leo ni 12 days sasa hakuna info yoyote....

Thanks na nawatakia sikukuu njema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Kutumia njia hizo ni kujizonga na ni kupoteza pesa tu, kutumia UPS au PARCELFORCE .

    Ushauri wangu wakati mwengine ukitaka kupeleka mzigo kutoka England to Zanzibar wasiliana na mie nitakufahamisha njia gani utumie.

    Na mzigo wako utafika Zanzibar ndani ya week moja

    ReplyDelete
  2. mama angu hizo ndio kero za muungano natumai katika katiba mpya yatakwisha

    ReplyDelete
  3. Ni kweli mizigo inayotumwa na makampuni ya excess luggage, door to door, na mengi mwisho ni Dar hata ukisema ipelekwe Zanzibar. Isipokuwa kama utatumia shirika la ndege la Kenya Airways ndio utafikishiwa Zanzibar. Nafikiri hii ni kero ya Muungano. Makampuni mengi ya uchukuzi wanakufikishia mzigo "First Entry" ya nchi yako. Kwa maana nyengine wanakuibia.

    ReplyDelete
  4. Mfumo huo hayawezi kwisha hadi zanzibar iwe nchi nalo mpaka damu imwagike apatikane rais mwenye uchungu na nchi

    ReplyDelete
  5. wewe annon hapo juu huna jipya..hizo kero za muungano zimeingia hapo??Ni UPS ndo tatizo coz hawana ofisi Znz sasa muungano umeingia hapo???usikute kwa mwaka wanapata ni hako kamzigo kamoja tu ka kwenda Znz sasa ndo maana wanaona hakuna umuhimu wowote wa kufungua ofisi huko...

    ReplyDelete
  6. Wapinga Muungano,

    Hata huko Oman kwa Mtawala wa Zanzibar hakukosekani changamoto za mambo kadha wa kadha, Mafano suala dogo hili la Usafirishaji Mizigo!

    Kama Oman iliyo jitawala na kutowahi Kutawaliwa kama Zanzibar ingekuwa peponi nadhani wasingekuwa na Shida kuwekeza Tanzania ktk Shirika letu la ndege la ATCL !

    Mpo hapo akina Makame?

    ReplyDelete
  7. Wadau wa 2, wa 3 na wa 4 NINYI WENYE MSIMAMO WA KUKEREKA NA MUUNGANO.

    SUALA LA UTUMAJI WA PERCEL NDIO SABABU YA MJADALA WA MAPUNGUFU YA MUUNGANO?...KAMA HILO NI TATIZO MAPENDEKEZO NA MADAI KWENYE KATIBA MPYA MTAREKEBISHIWA.

    JE, HUYO MWENYE UCHUNGU NA NCHI ZAIDI YA RAISI WA ZANZIBAR ALIYEPO SASA ATAKUWA NANI?, AU NINYI?

    TAARIFA KAMILI:

    MUUNGANO HAUVUNJIKI!

    KWA ''MENTALITY'' YENU AMA MSIMAMO WENU NINYI NO.2, NO.3 NA NO.4 KAMWE HAMUWEZI KUUPATA URAISI WA ZANZIBAR HATA MZIKIRI UCHI!

    KAMA MKIWEZA KUJILAWITI NINYI WENYEWE NDIO MUUNGANO UTAWEZEKANA KUVUNJIKA NA KAMA HAMTAWEZA ZOEZI HILO NA PIA MUUNGANO HAUTAWEZA KUVUNJIKA!

    ReplyDelete
  8. Mkiitwa kutoa Mapendekezo ya Katiba Mpya ya ''JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA'' mpo Busy Uingereza mnabeba Maboksi!

    Leo tena ndio ninyi ninyi mnalalamika!

    Zaidi ya hapo wengi mnao lalamikia mambo humu hata Uzanzibari wenyewe na Utanzania milishaukana zamaniii kwa Kujilipua kwenye Ukimbizi!

    Madai yenu Mtoe kwenye Serikali yenu ya Ukimbizini huko huko Uingereza na sio kwa Dr.Shein na Dr. Jakaya Kikwete.

    Mbebwe vipi?

    ReplyDelete
  9. mpaka utukane blog hii inasomwa na watu wenye heshma tujizuie na matusi

    ReplyDelete
  10. hivi mmetoa ufumbuzi au mawazo au mmeingia kwenye Siasa

    Posta na simu ni suala la Muungano na hili pia ni jambo muhimu sana kwa Manufaa ya Zanzibar inakosa wawekezaji kwa kuwa wanashindwa kwa complexity zilizo TRA Bara.

    Si dhani kuwa asilimia(%) ya watumaji vitu hata ukiangalia data za kihistoria utakuwa Wazanzibari ni wenye kutuma vitu sana na wamechangamka kibiashara na Watanganyika ni followers tu

    ila Kwa vile wanabaniwa ndio inakuwa tabu hili ni jambo muhimu sana liangaliwe.....
    The only way ni Kutumia CONDOR AIR hapo mzigo moja kwa moja ZNZ kila jumatatu....

    Na huyo alosema kujiripua kwani mkimbizi si wa kukukosoa pia au unataka aje mzungu kabisa ndio akukosoe....kama wewe hujawa na uwezo wa kuruka kwa siasa zako za CCM basi bakia huko huko.....
    Goodluck

    ReplyDelete
  11. ndugu zangu mnakosa hekima mjadala hapa ni shida na upokeaji wa hivyo vijifurushi vyenu,sasa matusi yanatoka wapi sasa nasema hivi hii tanzania haitavunjika muungano wake hadi yesu kristo atakaporudi kwa mara ya pili,pia msiingize mambo ya siasa zisizo na maana kwenye mijadala ya maana. habari ndiyo hiyo.

    ReplyDelete
  12. Watu wengine bwana wanachekesha ati hii sio hoja ya Muungano au ati ZNZ hakuna wanaotuma mizigo ndo maana UPS hawana office

    Hebu jiulize kwa nini Zantel wakakimbia kutoka ZNZ? sasa unafikiri UPS nao wajinga wataenda ZNZ wakalipe duel Taxes ?

    Muekezaji yoyote ni Suala la Muungano ataoewaje kibali na ZNZ ?
    Posta na Simu ni kero iloingizwa kinyemela kwenye Muungano
    Ushuru mambo ya Muungano

    Sasa kama hili si la muungano kwa nini wasiutue tu hiyo mizigo moja kwa moja ZNZ ? na WALE TRA wanakazi gani kule kama hili si la Muungano.....
    mtu akiwa TZ kweli ni Shaban Robert aliwaona nyie katika KUSADIKIKA....BADILIKENI TANGANYIKA

    ReplyDelete
  13. Ukweli ni kuwa mizigo inaletwa Zanzibar kwa kutumia Door to door, UPS, Excess luggage, na wengi wengineo hufikisha Dar ambako ndio kwenye Agent wao. Sasa huyu Agent anakutumia email au fax kuwa mzigo wako umeshafika Dar airport ukachukue. Huyu Agent anatakiwa akuletee Zanzibar lakini hafanyi hivyo. Pale dar mzigo unawekwa Swissport(Darhako?) sasa inabidi ulipe storage, customs ndio upate mzigo wako. Kosa lipo kwa huyu Agent wao ambaye anataka kubana matumizi. Dar hakuna UPS bali agent wao tu.

    ReplyDelete
  14. Kwani ukiagizia mzigo kwa ups au dhl ukiwa nachingwea utaletewa mlangoni? Sio tatizo la muungano. Ni mambo ya kibiashara tu

    ReplyDelete
  15. Hivi wajameni mada hapa ni nini hasa??

    ReplyDelete
  16. mdau hapo juu uko na mie kifikra. Maada ni ipi hapa

    ReplyDelete
  17. Mimi naona mtoa mada anajichanganya
    Kwanza anadai mzigo hauna thamani(?), baadae anataja thamani(?!)
    Anaendelea kujichanganya pale anahusisha utumaji wa mzigo wake na TRA, TRA hawahusiki kabisa na utumaji wa mzigo bali wanahusika endapo mzigo unahitaji kulipiwa kodi.
    Mtoa hakufanya utafiti wa kutosha ni kampuni gani itafikisha mzigo wake kwenye address aliyoweka, endapo mkataba wake na UPS wakati wa kutuma mzigo umeeleza wazi utafikishwa Znz, basi sioni kwanini ameandika hii post ilhali ana makubaliano na UPS?
    Rudi kwa UPS ukalalamike na TRA au Muungano.

    ReplyDelete
  18. Hawa ndio Watanzania Mtu anahitaji msaada, wao kulumbana. Hebu mie kidole gumba.

    Mdau wabane hao UPS

    ReplyDelete
  19. Anoy wa 27DEC 13 nadhani wewe ndio unajichanganya Mtoa mada ameeleza kwa uwazi kabisa Je TRA hawafanyi kazi ZNZ? ngoja nikusaidie hivi wewe unakaa Scotland kwa vile BA inatua kwanza London Heathrow unadhani ni Sahihi mzigo wako ushushwe pale kisha uambiwe toka Scotland njoo London kwa sababu yote ni U.K? HIVI KULE SCOTLAND HAKUNA REVENUE DEPARTMENT...
    nimeelewa sawa sawa hii mada tatizo hapa ni TRA n UPS kwa kuwa ukisoma maelezo ya TRA kifungu kimmeandikwa uzuri kabisa kuwa MIZIGO YOTE YA ZNZ basi FORWARD Documents zote ZNZ isiingizwe kwenye file za DAR...
    Sasa hivi hawa TRA wanashindwa kujua kwamba document zimeandikwa ZNZ hata kama yote ni TANZANIA? kwani TRA kuna makubaliano ya POINT OF ENTRY ndio ulipwe ushuru na kama ni hivo mbona wanasema gari ikija BARA ILIPIWE DIFFERENCE...?
    kumbuka hii ni door to door service mbona dhl wanafikisha ZNZ na unalipa kule kila kitu?

    Ama kuhusu thamani imesemwa hapo kuwa Ni free gift sasa kama wewe una thamani yako msaidie mtoa mada kama huna la kusema nyamaza

    ReplyDelete
  20. Ingelikua hakuna muungano hii mada isingekuepo hapa, kila mtu kivyake - muungano ni kero. Mzigo wa Zanzibar unaishiaje Dar, mbona hawakuupeleka Kenya ama Uganda!

    ReplyDelete
  21. Jamani naomba katika hili mnisaidie na mimi, nimesoma vitabu vingi na malalamiko mengi ya Wazanzibar lakini sioni hasara ya kuvunja Muungano. Hivi Muungano ukivunjika watanganyika tunapoteza nini? - Wacha uvunjike tu ili tupumue

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...