katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na ujumbe wake wakizungumza na Wafanyakazi wa TAZARA-Iyunga,Wilayani Mbeya mjini Mkoani Mbeya mapema leo,kuhusiana na changamoto mbalimbali yanayoikabiri shirika hilo nchini.
Kinana alisikiliza changamoto mbalimbali kutoka kwa Uongozi wa Shirikia hilo ikiwemo suala la Uchakavu wa mitambo na vitendea kazi,Upatikanaji wa Mafuta ya kuendeshea mitambo,Upungufu wa wafanyakazi,Kutolipwa Mishaharaya Wafanyakazi kwa wakati,Makato ya malimbikizo Michango ya Wafanyakazi kupeleka NSSF,Mafao kuchukua mda mrefu,Hujuma mbalimbali ndani ya shirika hilo, ukosefu wa magari na changamoto nyinginezo.
Ndugu Kinana katika kujibu na kutoa ufafanuzi wa changamoto hizo,alizipokea na kuomba kuzifanyika kazi ipasavyo na kuhakikisha TAZARA inaimarika.Aidha aliongeza kwa kusema kuwa kuna baadhi ya Changamoto zinatokana na baadhi ya wenye Malori kufanya hujuma mbalimbali kuhakikisha TAZARA inaendelea kudidimika kila kukicha,kwamba hawapendi TAZARA ifufuke,Kwa hivyo tutafute namna ya kuimarisha TAZARA
Wafanyakazi wa Shirika la TAZARA wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao mapema leo,kwenye ukumbi wa mikutano wa shirika hilo mara alipowasili na ujumbe wake kutokea Mbeya Vijijini katika ziara ya kukiimarisha chama cha CCM.
Mmoja wa wafanyakazi wa TAZARA,aliyejitambulisha kwa jina la Maulid Said akzizungumza kuhusiana na hujuma mbalimbali zinazofanywa na baadhi ya watu ya kuhakikisha shirika hilo haliendelei,aidha ameitupia lawama Serikali kwa kuacha barabara zetu zikiharibika kila kukicha na Malori ya Mizigo kwa kuzidisha uzito huku ikishindwa kuliimarisha shirika la TAZARA ambalo lingeweza kupunguza ama kuliondoa kabisa tatizo hilo.
Mfanyakazi wa TAZARA,aliyejitambulisha kwa jina la Seif Rashid akiuliza swali kuhusu suala la Mafao katika shirika hilo la TAZARA,akibainisha kuwa limekuwa tatizo sugu kwa Wafanyakazi wastaafu.
Mmwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wilaya (Mbeya) TAZARA,Ali Mkami akisoma hotuba fupi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM na Ujumbe wake uliofika kwenye shirika hilo na kuzisikiliza kero na changamoto mbalimbali zilizopo.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoani Mbeya Mary Mwanjelwa akiwasalimia Wafanyakazi wa TAZARA waliofika kuzungumza na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake,akiwemo Katika wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro.Ndugu Kinana na Ujumbe wake leo wako Mbeya mjini kuhitimiza ziara yao ya Kuimarisha chama cha CCM,Ziara hiyo ilianzia Mkoa wa Ruvuma na Mbeya na Njombe.
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...