Leo ni siku ya mwisho ya kuaga mwili wa Mzee Madiba kabla ya kusafirishwa kuelekea kijijini kwake Qunu kwa mazishi siku ya Jumapili. Mitaa ya mji mkuu wa Afrika Kusini, Pretoria, bado imefurika maelfu ya waombolezaji wakiwa katika foleni ndefu kwenda kuamuaga Tata Madiba. Wengine wanaimba na kucheza kusherehekea maisha ya Nelson Mandela, Rais wa Kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini. Globu ya Jamii ipo eneo la tukio na Libeneke litaendelea hadi mazikoni kijijini Qunu.
Home
Unlabelled
LEO NI SIKU YA MWISHO KUAGA MWILI WA MADIBA HAPA PRETORIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...