Mzee Mandela na mkewe Winnie Mandela wakiwasili Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam mwaka 1990, siku chache baada ya Madiba kuachiliwa huru kutoka gerezani na kabla hajawa Rais wa Afrika ya Kusini. Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza kuitembelea baada ya kuachiwa huru ikiwa ni kutoa shukrani kwa msaada wa hali na mali aliopokea toka Tanzania wakati wa kugombea ukombozi wa Afrika Kusini
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere akiwatambulisha Nelson Mandela na Winnie Mandela kwa Watanzania Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam mwaka huo wa 1990
Waziri Kiongozi wa Zanzibar wa wakati huo, Marehemu Dr. Omar Ali Juma, akiwalaki Madiba na Winnie Mandela walipotembelea visiwani mwaka huo wa 1990
Maelfu ya wananchi wa jiji la Dar es salaam walijitokeza kumlaki Nelson Mandela na Winnie Mandela alipotembelea Tanzania mara baada ya kutoka kifungoni mwaka 1990. Ankal, ambaye ndiye aliyenasa taswira zote hizi, anaikumbuka hii siku kama ya kihistoria kwake kwani ndio ilikuwa kazi yake kubwa ya kwanza toka ajiunge na gazeti la Daily News.
Tanzania hatukuanza harakati za Ukombozi leo hii kwa kutuma Vikosi Vitani Congo-DRC kuwasakaka Waasi!
ReplyDeleteRwanda na Uganda mliokereka na Operesheni ya Majeshi yetu JWTZ-UN BRIGADE huko DRC habari ndiyo hiyo, mtu wa UZAO wetu Jemadari Mpiganaji mwenzetu Mzee Madiba ndio huyooo ameaga dunia...Tanzania tunasikitika tunaomboleza!
Kama inavyoonekana Kidume Mzee Madiba anachomoka Lupango moja kwa moja anawaona Wapiganaji wenzake TANZANIA!