
Akizungumza na na kituo cha redio ya Nuru fm ya Iringa,kupitia kipindi cha sunrise power,Mh. MSIGWA amesema kuwa ni kweli pesa hizo alipokea kupitia kwa MAJID MGENGWA na baada ya kupokea fedha hizo alichangisha tena fedha kwa wananchi wa jimbo la Iringa mjini kupitia mkutano, ambapo walichangia kiasi cha laki tatu pamoja na yeye mwenyewe aliongezea kiasi cha shiringi laki tano ,hivyo kupelekea kufikia kiasi cha shiringi milioni moja na laki nane na sitini na nane na kumkabidhi mjane wa marehemu DAUDI MWANGOSI.
Msigwa amesema kuwa ni wanasiasa tu wanaojaribu kuwachafua baada ya kuona kuwa wameshindwa na tayari amewasiliana na uongozi wa chama chake ili kuweza kulichukulia hatua gazeti ambalo limeandika tuhuma hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...