Mshindi wa shindano la Mama Shujaa wa chakula mtandaoni
Neema Urasa Kivugo kutoka Kibaya Kiteto.akifurahia mara baada ya
kutangazwa usiku huu jijini Dar es salaam
Neema, ambaye amepata kura 778 kati ya kura 1011 ambayo ni sawa na asilimia 76.95 ya kura zote zilizopigwa, amejishindia vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Tshs. Milioni 5 ambavyo atachagua yeye mwenyewe na nafasi ya moja kwa moja ya kushiriki shindano kubwa la Mama Shujaa wa Chakula linalofanyika sambamba na kipindi cha Maisha halisia cha Maisha Plus litakalozinduliwa rasmi siku ya Jumanne tarehe 10/12/2013.
Shindano la Mama Shujaa wa Chakula mtandaoni lilifunguliwa rasmi tarehe 4/11/2013 na Balozi wa Kampeni ya Grow, mwanawavuti Shamim Mwasha kama mchango wake kwa wakulima wadogo wanawake.
Akiongea baada ya kutangazwa mshindi, Neema amelishukuru shirika la Oxfam kwa kufadhili shindano hilo na kwamba limemtia moyo kuendeleza kilimo na anaahidi kuwashirikisha wanawake wakulima wenzake.
Naye Shamim amewashukuru na kuwapongeza washiriki wote wa shindano hilo. Ametambua mchango wa wakulima wote hasa wanawake na kusema kwamba wote ni bora na wasivunjike moyo kwa sababu hawakushinda bali waendelee kuamini kwamba jamii inathamini sana mchango wao kwani chakula wanacholima ndicho tunachokula.
Washiriki waliobaki pia wana fursa ya kushiriki shindano kubwa la Mama Shujaa wa Chakula, kwa kujaza fomu, linalofanyika sambamba na kipindi cha maisha halisia cha Maisha Plus litakalozinduliwa rasmi siku ya Jumanne tarehe 10/12/2013.
Hafla hizo zilihudhuriwa na Bi. Anna Maembe, Katibu Mkuu wa Wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia na watoto, mabalozi wa kampeni ya GROW, washiriki watatu kati ya watano bora ambao ni Ezeline Mujila, Neema Urassa ambaye ni mshindi pamoja na Gloria Kidulile.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...