WAKATI maandalizi yam bio ndefu za Uhuru, Uhuru Marathon, yakiwa yamekamilika zawadi kwa washindi zimetangazwa upya pale mshindi wa mbio ndefu za kilomita 42 kwa upande wa wanaume na wanawake akiondoka na Sh milioni 2.

Huku mshindi huyo akiondoka na fedha hizo, kwa upande wa mbio za kilomita 21 kwa wanaume na wanawake kila mmoja ataondoka na Sh milioni 1, hivyo kuongeza chachu ya mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika kesho kwa kuanzia na kumalizikia katika Viwanja vya Leaders, vilivyopo Kinondoni, Dar es Salaama.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, Kaimu Mkuu wa Mkoa, Sophia Mjema alisema, wana faraja kubwa kwa maandalizi ya mbio hizo kukamilika na hivyo kutimiza azma ya kudumisha uhuru, amani, umoja na mshikamano uliopo miongoni mwa Watanzania.

“Tunachukua fursa hii pia kutoa shukrani za dhati kwa Rais Jakaya Kikwete kwa kukubali kwake kushiriki mbio hizo kwa mbio za kilomita 3. Hii inadhihirisha jinsi Rais Kikwete alivyoguswa mno na suala la kupigania amani, umoja na mshikamano miongoni mwetu.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...