KINYWAJI CHA WINDHOEK TANZANIA kilidhamini bonge la party la kusherekea miaka mitano ya Grooveback Djs ambayo inaundwa na ma DJ wakali na maarufu hapa nchini,ambao si wengine bali ni Dj Peter Moe,Dj PQ, Crucial, KT, Tony na JB. Party hiyo ambayo ilikuwa ni funga kazi na yakufungia Mwaka pia,ilifanyika jumamosi Desemba 28 katika bar maharufu ya East 24 Bar & Grill,Mikocheni jijini Dar es Salaam,huku Ma Dj wakali waalikwa waliokuwepo ni Dj Pinye na Dj Nijo wote kutoka nchini Kenya. Grooveback wanapiga disco la nguvu kila jumamosi katika kiota hicho cha East 24 Bar, Arcade House, chini ya udhamini wa Windhoek Lager – 100% PURE BEER.
Dj Peter Moe (pili kushoto) akilekezana jambo na mkali mwenzie toka nchini Kenya,Dj Pinye huku Dj PQ (kulia) akitupia macho.
Palikuwa hapatoshi ndani ya kiota cha East 24 Bar & Grill,Mikocheni jijini Dar es Salaam siku hiyo.
Mdau Jerome Rugemalila akishow love na Dj Pinye kutoka nchini Kenya wakati wa sherehe hiyo ya Grooveback Djs.
Dj. Peter Moe akifanya yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...