Wajasiriamali wapiga picha wakiwa kazini kwenye mnuso katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam hivi karibuni. Vijana wengi nchini kote wamejiajiri wenyewe katika shughuli hii na inaonesha mambo si mabaya sana
Wajasiriamali wengine ni wabunifu kwa kuwa na 'mali' adimu ya mbwa. Ukipita barabara ya New Bagamoyo Road maeneo ya Victoria jijin Dar es salaam unaweza kujipatia rafiki huyu kwa binadamu kwa bei ya maelewano, kutegemea umri na aina ya mbwa. Globu ya Jamii haikupata nafasi ya kuuliza 'chanzo' cha mali hai hii, huenda anafuga mwenyewe nyumbani...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Siku hizi kuna "Selfie" hivyo ajira yao ipo mashakani!!

    ReplyDelete
  2. Ohhh Mjomba Michuzi!

    Ungesema hawapo kwenye Ajira sema wanafanya Kazi kwa kujitolea na kupata hela kidogo ya kula kwa kuchangiwa na Wahisani, kwa kuwa Ndugu zetu Majuu MADIASPORA (ni waoga sana kwa mazingira yakazi zisizo na Mikataba na mafao makubwa kama hizi) tukiwaambia ya kuwa Uuzaji wa Mbwa na Kupiga picha na kuzitandaza chini (TENA BILA KUPEWA TENDA) NI KAZI ni kuwa watashutuka sana na kughairi nia za kurudi nyumbani Tanzania!

    Sema wanapiga Picha kama Wafanyakazi wanao jitolea ktk Minuso na kuchangiwa chochote wakale na wale wa uuzaji mbwa wanachangia ktk Ulinzi Shirikishi na kuchangiwa chochote nao wakale!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...