Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi –Zanzibar

Wananchi wa Shehia ya Mwanyanya nje kigogo ya mji wa Zanzibar wakiongozwa na Kikundi cha Vijana wa Green Society cha eneo hilo, wameshiriki katika kazi ya ukusanyaji na uzoaji wa taka katika shehia hiyo.

Wakizungumza mara baada ya kazi hiyo, Mwenyekiti wa Green Society Bw. Ali Abdallah Ali na Ali Bakari Khatibu, wamesema mbali ya kikundi hicho kushiriki katika kazi hiyo ya uzoaji taka, pia kikundi hicho kitaendelea na kazi ya ustawishaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na kupanda miti ya kisasa na kuitunza ile ya uwoto wa aslai iliyopo katika eneo hilo.

Wamesema Kikundi hicho cha Mwanyanya Green Society kitahakikisha kuwa kila kijana na mwananchi wa eneo hilo la Mwanyanaya anashiriki kwa hali na mali katika kazi za usafi wa mazingira na kulifanya eneo la Mwanyanaya kuwa lenye kijani kibichi na lisilokuwa na taka.

Awali Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Mazingira Zanzibar Bi. Zuwema Juma Hamadi, ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika shughuli hiyo, alisema kuwa ofisa yake imeanzisha operesheni ya uzuiaji wa uchimbaji wa mchanga kiholela ikiwa ni sehemu ya kuzuia uharibifu wa mazingira.

Vijana hao wa Green Society, wameitumia siku hiyo kama sehemu ya uzinduzi wa kikundi chao ambacho mbali ya kujihusisha na masuala ya ustawishaji wa mazingira pia kinalenga katika kumkwamua kijana katika matumizi ya dawa za kulevya na kumjengea mazingira ya kujiajiri.

Aidha Vijana hao wametoa wito kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kujitolea katika masuala ya usafi na usawishaji wa mazingira kwani kwa kufanya hivyo kutaiwezesha nchi yetu kuwa ya kijani kibichi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...