Abiria wa treni iliyokwama Dodoma wakiwa na watoto wao wakipata chochote wakati wakisubili hatima yao huku katika stesheni hiyo kukiwa hakutamaniki kwa uchafu unaotishia afya zao kutokana na abiria zaidi ya 1500 kutakiwa kutumia matundu manne ya vyoo.(Picha na John Banda)


 Wasafiri wa treni toka Kigoma na Mwanza kuelekea Morogoro na Dar es laam wakiwa wamelala kwenye mabehewa hawajui cha kufanya baada ya treni hiyo kushindwa kuondoka Dodoma kutokana na Maji kujaa relini Gulwe na Mzaganza.
 Abiria waliokuwa wakisafiri na treni kuanzia kigoma kwenda Dar es laam wakielekea kwenye ofisi ya mkuu wa stesheni ya Dodoma mara baada ya treni hiyo kukwama kuondoka kwa sababu ya mafuliko yaliyosababishwa na mvua maeneo ya Gulwe na Mzaganza.
 Abiria wakisongamana dirishani kupokea fedha za kujikimu 3500 zilizotolewa na shirika la reli baada train hiyo kukwama kuondoka Dodoma.

 Abiria hao wakiwa kwenye foleni kuelekea kwa mkuu wa stesheni ya Dodoma, Zacharia Kilombele ambako walikuwa wanapewa pesa ya kujikimu tsh. 3500 kwa abiria zaidi ya 1500 walikwama kutokana na mafuriko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. bado tuko kipindi cha ujima

    ReplyDelete
  2. Kama wameshafika Dodoma kwa nini shirika la reli lisikodishe mabasi kuwaleta dar badala ya kuwapa fedha za kujikimu? just a thought..

    ReplyDelete
  3. Ukisafiri kwa treni lazima ubebe chakula cha kutosha kula wiki maana hujuhi unafika lini na inakuwa inshu likizimikia porini...

    ReplyDelete
  4. Waziri Jembe Mwakyembe, haya hili lako sasa,, hebu kodisha mabasi yawalete hao watu Dar, maana hiyo reli hamtaki kuiboresha, au sijui ina laana maana sielewi kila siku reli ya kati reli ya kati

    ReplyDelete
  5. Tunakwenda wapi? miaka 30 niliyopita usingeona upuzi, leo tunajiita tumendelea , hayo maendeleo yapo wapi? tunashindea hata kusafirisha wananchi wetu waende majumbani kwao, Ikiwa miaka ya 60 hakukuwa na visa hivi je leo hii tunauhuru wa namna gani? Tunaelekea wapi? je tunawafunsidha nini jamii na familia zetu tunaishi maisha gani? elimu gani hao vijana wanosafiri na hiyo treni wanjifunza, Je unafikira nini? zamamni unatamani uwe mkubwa uje uwe conductor wa train au Dereva, au uje uwe Railway Inspector, leo hiivijana hata train hawaijui tena hakuna pa kujivunia, hii ni balaa kwa jamii yetu ya baadae. Tulipaswa hat tuweze kurekebisha hiyo mito ya kukalia lakini haiwezekani hta fundi wa mitaani anweza kufanya hiyo kazi, ina maana hatuna hata pesa ya kurekebisha hiyo miyo ya kukalia? Hii ni hatari sana, ina maana hao wakuu wa shiriki hawajahi kutembelea hayo mabehewa? inamaana wankaa offisini tu na kupokea Mshahara, na kama wanona shida kurekebisaha hata hiyo mito kwanini wainunuwe mabehewa ambayo hayana mito? Ina maana tunaviongozi wanokuja kunywa chai offisini na kula chakula cha machana na kurudi nyumbani.

    ReplyDelete
  6. Usilolijua ni sawa na usiku wa giza! Mafuriko ndo yalosabababisha haya yote haya, unawezaje kuzuia natural disasters? Kabla hatujatoa maoni ya kipumbavu yafaa kuelewa jambo kwanza. Au hawa abiria wangepelekwa porini wakaachwe hapo wakati mafundi wa kitengeneza reli!!??? watanzania wenzangu tupunguze kulalamika, midomo imetuzidia. We unaesema wapelekwe kwa mabasi, kampuni ya reli ina mabasi au unaropoka tu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...