Na Demetrius Njimbwi na Alexander Mpeka, Jeshi la Polisi
Kamishna wa Polisi Jamii Nchini, (CP) Mussa Alli Mussa, amewataka maofisa wa Polisi pamoja na askari kote nchini, kuhakikisha wanafanya kazi zao katika misingi ya uwazi na usasa, dhana itakayosaidia uenezi wa Polisi jamii/ulinzi shirikishi katika kupambana na matukio ya uhalifu na wahalifu.
Kauli hiyo ameitoa jana wakati alipokutana na baadhi ya watendaji wa Jeshi la Polisi katika wilaya ya kipolisi ya Ilala, katika kikao cha pamoja kuhusiana na utendaji wa Polisi katika dhana ya Polisi jamii na namna ambavyo Jeshi hilo linavyoweza kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwa pamoja na kushirikiana na wananchi na jinsi wanavyoshirikishwa.
Kamishna Mussa, aliongeza kuwa, tangu kuanzishwa kwa Polisi jamii/ulinzi shirikishi, mafanikio makubwa yameweza kufikiwa kwani mpaka sasa makundi kadhaa ya uhalifu yameweza kugundulika na kuchukuliwa hatua ikiwamo kuangamizwa ikiwa pamoja na wahusika kuchukuliwa hatua kali za kisheria, alisema.
Hata hivyo, Kamishna Mussa, aliwataka wananchi kuwathamini na kuwapa ushirikiano maofisa wa Polisi/Polisi Kata pamoja na vikundi vya Ulinzi Shirikishi hatua ambayo itasaidia kukabiliana na matukio ya uhalifu katika maeneo mbalimbali na kuifanya jamii kuishi kwa amani pasipo kuwepo kwa matukio hatarishi.
Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Lazaro Mambosasa, alisema kuwa, Jeshi l Polisi limejipanga katika kukabiliana na aina zote za uhalifu na kwamba alitamuonea ama kumdhurumu mtu yeyote katika kusimamia na kulinda usalama wa raia na mali zao.
Mambosasa, ameongeza kuwa, kila askari katika nafasi yake anawajibu wa kuhakikisha kuwa, jamii inaondokana na uhalifu pamoja na matishiona huku akiwataka maofisa na askari kuwa na utayari katika kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia dhana ya Polisi Jamii/Ulinzi shirikishi, alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...