NA ABDULAZIZ VIDEO,Kilwa 
Halmashauri ya wilaya ya Kilwa imeomba kuidhinishiwa jumla ya Tshs 28,729,895,535 kwa ajili ya Uendeshaji wa shughuli mbalimbali za serikali ikiwemo Mishahara Tshs 14,016,723,484 huku mapato ya ndani ni Tshs 268,112,400 na matumizi mengineyo (OC)ni 1,567,578,000 toka serikali kuu na mapato ya ndani 2,054,184,359 
Aidha Miradi ya maendeleo tshs 2,994,804,988 toka serikali kuu na wahisani 409,817.075 na mapato ya ndani Tshs 10,823,297,292 Akisoma bajeti hiyo katika kikao cha Baraza maalum la bajeti kwa Madiwani wa Halmashauri hiyo,Afisa Mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa,Daniel Lusingu alibainisha kuwa Bajeti hiyo ina ongezeko la jumla ya Tshs 8.866,528,435 sawa na asilimia 44.63 ya bajeti ya mwaka 2013/2014 
Pamoja na maombi hayo ya kuidhinishiwa mapato na matumizi Halmashauri ya wilaya ya Kilwa katika kuhakikisha inaongeza mapato kutoka katika vyanzo vya ndani imejipanga kuongeza wigo baada ya kubuni vyanzo vipya ikiwemo kuongeza wigo wa ukusanyaji kodi mbalimbali, Kuimarisha Uagizaji na utunzaji wa nyaraka za kukusanyia mapato na kuimarisha rejesta ya vyanzo vya mapato Sambamba na kuongeza wigo wa ubinafsishaji wa vyanzo na kufanya uhakiki kila mara pamoja na kutoa elimu kwa walipa kodi na kuongeza nguvu kwenye kudhibiti mazao yatokanayo na bahari,kilimo na misitu kwa kusimamia kwa karibu vizuizi katika maeneo ya Singino,Migeregere,Mbwemkuru,mihangalaya na Nanjirinji 
Akichangia bajeti hiyo,Diwani wa kata ya Songosongo,Mhe Hassan Swaleh pamoja na kuunga mkono Bajeti hiyo aliiomba Halmashauri hiyo kuona umuhimu wa kuthamini wavuvi kwa kupatiwa zana bora za uvuvi Ili kuongeza wigo katika makusanyo ya baharini
Madiwani wakiwa katika kikao cha kupitisha bajeti kinachoendelea katika ukumbi wa Jumba la maendeleo wilayani Kilwa
Madiwani wakiwa katika kikao cha kupitisha bajeti kinachoendelea katika ukumbi wa Jumba la maendeleo wilayani Kilwa
Afisa Mipango wa Halmashauri ya wilaya ya kilwa ,Daniel Lusingu akiwasilisha makisio ya bajeti ya Halmashauri hiyo
Wakuu wa Idara wa Halmashauri wakihudhuria kikao hicho

Meza Kuu. Picha zote na Abdulaziz Video

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...