JANUARI 2, mwaka huu Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, ilitoa zuio la muda kwa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutojadili uanachama wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mhe Zitto Kabwe katika kikao cha chake cha Januari 3, mwaka huu.
Januari 3, mwaka huu mahakama hiyo ilisikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili kuhusu maombi hayo mbele ya Jaji John Utamwa.
Januari 7, mwaka 2014, mahakama hiyo pia ilitoa amri kwamba Zitto asijadiliwe uana chama wake hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.
Mhe Zitto alikuwa anatetewa na wakili Mhe Albert Msando na Chadema walikuwa wanawakilishwa na Mhe Tundu Lisu na Mhe Peter Kibatala.
Katika kesi ya msingi, Zitto amefungua kesi dhidi ya Baraza la Wadhamini la Chama hicho na Katibu Mkuu, Willbrod Slaa, akiiomba Mahakama itoe zuio la muda la Kamati Kuu kutojadili suala la uanachama wake hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi na mahakama hiyo.
Katika maombi yake, Zitto anaiomba mahakama kuiamuru kamati kuu na chombo chochote kisijadili uanachama wake hadi rufaa yake itakaposikilizwa katika Baraza Kuu la Chama.
Kadhalika, anaoimba mahakama imwamuru, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa kumkabidhi nakala za taarifa na mwenendo mzima wa vikao vilivyomvua uongozi ili akate rufaa katika ngazi ya juu ya chama hicho.
Mhe. Zitto kupitia wakili wake Msando aliomba mahakama itoe zuio la muda la Kamati Kuu na vikao vingine vya chama kutojadili suala la uanachama wake hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Akiwasilisha hoja zake wakili Msando aliomba zuio hilo litolewe hadi Zitto atakapopata nafasi ya kuwasilisha rufaa yake ya kupinga uamuzi wa kumvua uongozi katika chama, uliotolewa katika kikao kilichofanyika Novemba 12 mwaka 2013.
Wakili Huyo alidai endapo amri hiyo haitatolewa na Kamati Kuu ikamvua uanachama, Zitto atapata athari kubwa kuliko chama chenyewe kwa kuwa atapoteza nafasi yake ya ubunge na kushindwa kuwatumikia wananchi waliomchagua.
Pia, mwanasheria huyo alidai athari nyingine ni kwamba iwapo atafukuzwa uanachama, Zitto atapoteza nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).
Alisisitiza kuwa, Zitto haizuii Chadema kufanyakazi zake za kisiasa kama wao wanavyodai katika hati ya kiapo kinzani, bali anaomba Kamati Kuu isijadili suala lake la uanachama mpaka uamuzi utakapotolewa.
Akijibu hoja hizo Wakili wa Chadema, Mhe Lissu alidai kuwa katika kutoa zuio la muda mahakama inatakiwa iangalie maslahi ya walio wengi na si faida ya watu wachache.
Alidai katika hati ya kiapo, Mhe Zitto anadai hakuna tarehe ya kikao cha Baraza Kuu la chama kilichopangwa, pia asipokata rufaa hatotendewa haki na atapata madhara lakini dawa ya woga na hofu yake ni kuomba mahakama iamuru kikao cha Baraza Kuu kifanyike na siyo kuomba zuio.
Mhe Lissu alidai kuvuliwa uanachama kwa Zitto hakutakuwa na athari kubwa kama anavyodai, na kwamba athari atayoipata yeye ni kukosa posho na mishahara.
Baada ya kurejea vifungu mbalimbali vya sheria, kanuni, amri na uamuzi wa kesi mbalimbali za Mahakama Kuu, Mahakama ya Rufani na za nje, Jaji Utamwa alisema anakubaliana mtoa maombi.
“Kwa hiyo ninatoa zuio la muda kwa Kamati Kuu ya Chadema na au chombo chake chochote cha uamuzi kwamba kisimjadili na kutoa uamuzi wowote dhidi ya mleta maombi kuhusiana na uanachama wake kusubiri kusikilizwa na kuamuriwa kwa kesi yake ya msingi,” alisema Jaji Utamwa.
Kesi ya msingi inatarajiwa kutajwa Februari 13, mwaka huu.
Nimeangalia video ya mahojiana ya waandishi wa habari na mawakili wa CDM ilibidi nicheke. haw mawakili wenyewe kweli hata hiyo elimu dunia ya sheria bure tuu. Kweli unaweza kumwambia jaji kuwa kesi liisha saa 12:30 jioni na ukatakiwa uwakilishe kiapo kesho yake saa 2:30 asubuhi ukashidwa kwa sababu ya kutoweza kuwasiliana na Dr Slaa na hao wadhamini. Hawa mawakili walikuwa na muda wa kutosha kuandaa kiapo, kuemail kwa wahusika ambao wangesign na kuscan hicho kiapo na kuwaemail hao mawakili. Na kama jaji angegoma uhalali wa kiapo wanheomba video comference. Wakubali wasikubali wameshidwa kwa technicality na sidhani kama wako competent. Ubishi wa kisheria sio kuropoka lazima uwe ne precedents na hizo hazipatikani bila ya kudurusu kesi zilizopita. Walikurupuka wakidhania mahakama kuu ni ya Swai. Watake wasitake hatima ya ZZK itatolewa na na umma wa baraza kuu la CDN na sio kamati kuu inayokutana sebuleni kwa DR Slaa. Kama kweli ZZK ni mhaini pelekeni Baraza Kuu hoja zenu ili haki itendeke mnachoogopa nini? Bao la pili na la la ushindi la ZZK ni pale atakaposimamisha kamati kuu na vikao vyote vya CDM mpka rufani yake isikilizwe kwanza na mwisho ndio atakapogombea uenyekiti CDM na kuwaacha midomo wazi. Inabidi tuu wakubali kuwa siasa za kinafiki hazina nafasi tena. Mfano rahisi tuu kwa Dr Slaa, mbona Mandela alikuwa raisi kwanza kabla ya Thabo Mbeki, Hillary Clinton alimwaga manyanga kwa Obama, Zitto nyota inamwakia na this is his time.
ReplyDeleteKweli kabisa CHADEMA wakubali kumpisha Zitto kuwa mwenyekiti kunusuru chama chao. Ukweli wa mambo watanzania wanaitaji demokrasia ya kweli kupitia hivi vyama vya kisiasa na sio siasa za kinafiki kama kweli wanataka kuiondoa CCM madarakani. Hizi zote ni njaa na hizo ruzuku ndio chimbiko la migogoro. I nabidi sheria itungwe ili kuthibiti matumizi ya hizo ruzuku kuliko kuishia kwa viongozi tuu. Huku US viongozi wanakosa kazi kutokana na hizo ruzuku kutumika kwa matumizi yao binafsi. tatizo la demokrasia kwenye vyama bongo ni ruzuku tuu.
ReplyDeleteANASEMA ATHARI KWA ZITO NI MISHAHARA NA POSHO? hawaoni wananchi na watz anaowatumikia? Wanataka wamkoseshe sifa ya kuwepo PAC ili waendelee kutafuna bila maelezo. Halafu hili la PAC linamkera sana LISSU,kila anapohojiwa lazima alitaje. ZZK amewagusa. ZZK kaza buti na huyo mwanasheria ambaye anonekana jina lake dogo ila ni kichwa. Achana na lissu ambaye yeye ni mwanasheria na anavaa vyeo vya uzungumzaji wa CDM.Hivi CDM hakuna mzungumzaji wa Chama? HAWAJAJIPANGA,TUKIWAPA KURA WATANZANIA TUTAPOTEZA. BELIEVE ME.
ReplyDeleteAny way, but cdm not well prepared, equiped with leaders' trait. may be after 30 yrs. plz acheni siasa za majungu na vurugu. tuchezeni salama.
ReplyDeletewakili wa chadema ni bishoo tu sijui uhalali wa degree ya sheria walipataje na njia ipi,kibatala kazi ni kuonekana kwenye T.V tu anataka, kesi gani ameshida ajieleze zaidi ya kupata dhamana ya kesi zake zilizopita ambapo dhamana ni haki ya mshtakiwa katika kesi nyingi,isipokua murder,na armed robbery.
ReplyDelete