Wafanyabiashara  jijini Dar es salaam  leo wamefunga maduka yao kwa kile kinachodaiwa kugomea  mashine za risit za EFD toka TRA. Taswira hizi ni sehemu ya maduka hayo maeneo ya Kariakoo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Kwani lazima wafanye biashara? Kama hawataki kwanini wanabembelezwa? Na sisi wafanayakazi tunaolipa kodi bila hata majadiliano tungegoma ingekuwaje? muda wa kudekeana hamna ikiwa kweli tunataka maendeleo.

    ReplyDelete
  2. Mdau nakuunga mkono na miguu. Hawa wamezoea kuchezea simba sharubu. Serikali hapa igangamale. Kama mashine hizo ni bei ya juu itafutwe namna ya kuwafanya walipe taratibu na sio kwa mkupuo. Ila mambo haya ya kuambiana hawazitaki na wanataka walipe kodi kivyao ikome! Dawa ni kunyang'anya leseni kwa aliye kichwa ngumu. Bahati humu hamruhusiwi kuchafua hali ya hewa, vinginevyo ningepiga bonge la ushuzi.

    ReplyDelete
  3. Kwani hio kodi ya VAT wanalipa wao au sisi walaji? Mbona mikwala miingi?

    ReplyDelete
  4. hivi hawa si wanagoma mara ya pili hii au kumbukumbu yangu inanipotea?

    ReplyDelete
  5. nilisikia kipindi Fulani mbunge mmoja wa mbeya kama sikosei akitoa hoja bungeni kuhusu swala hili la mshine kwamba:

    1) Wanauziwa mashine kwa gharama kubwa wakati gharama halisi ni ndogo sana. Gharama halisi ni kama dola 200 wakati wao wanauziwa kwa gharama karibu milioni moja

    2) Machine hizi zinatumia risit maalum ambazo nazo zinauzwa kwa bei mbya. Mfanya biashara wa kati anaweza kutumia hadi 250,000 kwa siku kununua hizo karatasi za risiti. Mengine nimesahau. Nashauri wafanya biashara wasikilizwe tatizo ni nini labda kuna ufisadi katika ununuzi wa hizo machine.

    ReplyDelete
  6. Mimi naona utaratibu wa zamani(Risti za vitabu) uendelee kutumika na iundwe tume ya kuchunguza chanzo ni nini(Utani)

    David V

    ReplyDelete
  7. nyie mnaowalaumu wafanya biashara mnakosea mngefanya utafiti kabla kulaumu

    ReplyDelete
  8. Kuna ukiritimba hapo wa mashine. Waziri muhusika na TRA watupe ukweli!!

    ReplyDelete
  9. wachukue taimu tu hao wafanya biashara. Mimi natumia mashine miaka miwili sasa, ili ammount niliotumia kununulia imekuwa deducted kwenye VAT collections zangu na hio roll ya karatasi bei ya kawaida tu. Tusipende shortcuts kwenye kila kitu. Mbongo kajengewa Machinga complex anaishia kuuza biashara nje ya complex with an excuse ya wateja hawapandi, kwahio na mimi nihamishie ofisi yangu ya clearing kituoni posta??

    ReplyDelete
  10. wamezoea kukwepa kodi,hawazitaki kwa sababu zimeunganishwa kwenye mtandao wa TRA kutakua na uwezo wa kuwafuatilia.
    Nchi zote zilizoendelea wanatumia hizi machine na ukwepaji wa kodi unakua ni mdogo sana.asiekua na uwezo wa kununua afunge duka atafute kazi nyingine ya kufanya

    ReplyDelete
  11. Tunawalaumu na hatufanyi risechi kwa sababu hatuna imani yao...Tumeshawazoea kwa tabia yao ya kutukata VAT na kutia mfukoni...

    Kwa watu kama mie ambaye nakatwa kodi ya maana na serikali toka kwenye mshahara wangu siwezi ku sapoti hatua yoyote inayohusisha kuendelea kukwepa kodi kwa hawa wafanya biashara....

    Huu ukwepaji kodi na ukomeshwe kabisaaaaaa....

    Kama hizo mashine ni mradi wa vigogo nao washugulikiwe...sina hururma ikija kwenye suala la kodi

    ReplyDelete
  12. SIKU YA JUMANNE TAREHE 7 KWENYE MOJA YA VITUO VYA TELEVISHENI MOJA YA MAKAMPUNI YANAYOUZA MASHINE HIZO KUPITIA MSEMAJI WAKE ALISEMA BEI YA MASHINE MOJA NI SHILINGI LAKI SITA NA NUSU WAKATI TRA INASEMA BEI YA MASHINE HIYO NI SHILINGI LAKI NANE! BAADAYE TRA HAOHAO BAADA YA MIGOMO WAKAJA NA BEI YA SHILINGI LAKI SITA! HAPA NYIE MNAOJIFANYA WAZALENDO UCHWARA NA TRA MTUPE MAJIBU, KWANI HIZO KODI MNAZOLIPA KWENYE MISHAHARA YENU HUWA ZINABADILIKA HIVI KILA MWEZI? PILI KWANINI NIKIFUNGA BIASHARA SIRUHUSIWI KUMUUZIA MTU MWINGINE MASHINE HIYO? KWANI DATA ZINAZOWEKWA KWENYE MASHINE HIYO HAZIWEZI KUBADILISHWA? MBONA KOMPYUTA ZILIZOTUMIKA ZINAUZWA. NI WAZI KUNAUCHAKACHUAJI MKUBWA NA USIRI KATI YA SERIKALI,TRA NA WAUZAJI WA MASHINE HIZO.

    ReplyDelete
  13. Kuna kitu cha kuongeza. Inasemekana wanaopata nafasi ya kukadiria kodi nje ya uwepo wa mashine hizi wanaona zitawaondolea ulaji hivyo wanawaunga mkono wezi wenzao! Serikali igangamale na ikibidi wanyang'anywe leseni kwa kukataa kutozwa kodi. Hawa ni mafisadi kama mafisadi wengine tu !

    sesophy

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...