Wateja wa Vodacom sasa kufurahia Dabo Dabo kwa kupata dk. 40 za muda wa maongezi wikiendi hii na hiyo yote ni kutokana na kuzinduliwa kwa promosheni ya vifurushi vya wiki.

Akizungumzia juu ya promosheni hiyo, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa amesema, “wateja wetu watapata muda wa maongezi wad k 40 kupiga ndani ya mtandao na pia wataweza kupata sms 250 na vilevlie vifurushi vya intaneti yenye kasi ya MB 100 wikiendi nzima”.

“Promosheni hii iliyopewa jina la Dabodabo itafikia kikomo wikiendi hii ya Januari 12, hivyo nawataka wateja wetu waitumie ipasavyo kwa kuwasiliana na ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wapendwa wao.” Alisema Twisa na kuongeza

“Mbali na hayo ningependa kuchukua nafasi hii kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutuunga mkono kwa miaka mingi sasa, na hicho ndicho kilichotupelekea kuwaletea promosheni hii kama ishara ya shukrani zetu kwao. Zaidi ya hapo kuna ofa, huduma na bidhaa kemkem zipo njiani zinakuja kwa ajili yao.” Alisema

Ili kujiunga na promosheni hiyo mteja anatakiwa kupiga *149*01# au *147*500#

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...