Baadhi ya wanafunzi wa halaiki wa skuli mbali mbali za Zanzibar na Tanzania Bara wakijiandaa kwa ajili ya sherehe za mapinduzi ifikapo Januari 12 mwaka huu wa 2014.
Gari za Polisi zinazotumika wakati wa fujo na vurugu katika maeneo mbali mbali nchini zikiwa katika matayarisho ya mwisho kwa ajili ya sherehe za kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar zitakazofanyika huko uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.
Makomandoo  wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ } wakionyesha umwamba wao wakati wa matayarisho ya mwisho ya maadhimisho ya kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kifaru cha kivita cha JWTZ kikifanya matayarisho ya mwisho kwa ajili ya maadhimisho ya kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar zinazotarajiwa kufanyika uwanjani hapo Jumapili ya Januari 12 mwaka 2014.
Askari wastaafu wa Jeshi la Ukombozi la Unguja { JLU } ambalo linatarajiwa kuonyesha vitu vyao wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Wapiganaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakionyesha ustadi wao wakati wa mazoezi ya mwisho kwa ajili ya sherehe za kutimia nusu karne ya mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964. 
 Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kumbe na sisi tunao 'navy seal'. Safi sana vijana.

    ReplyDelete
  2. Baada ya Congo DRC ,safari hii wakati Maamuzi ya mgogoro wa ziwa yakisubiriwa hawa vijana wa JWTZ-Tanzania Brigade watumwe kidogo Malawi !

    Maana Bundi ameunguruma kwa mama Joyce Banda kulidai ziwa Nyasa.

    ReplyDelete
  3. Vijana Wapiganaji wa JWTZ ninawakubali sana tu!

    Katika mchakato wa kuchukuliwa alama za vidole na picha kwa Vitambulisho vya Taifa kwenye eneo langu la makazi, ilipotimia siku yetu wakazi tulijidamka kuwahi nafasi na huduma.

    Katika hali ya kustaajabu tuliwakuta Vijana wa JWTZ wameshafika na kushusha vifaa kabla hata ya saa 12 asubuhi!

    Tuliwakuta wanapanga vifaa kwa nidhamu ya hali ya juu na utulivu wakiwa makini sana, ambapo hadi saa moja kasoro robo wamemaliza wakawaachia Polisi kulinda wao wakaparamia Lori lao wakaondoka.

    Jambo la ajabu Vijana wa Kiraia Makarani wakatuweka hadi saa 3 asubuhi!,,, wanaingia saa 3.30 kila mtu alikuwa amefura kwa hasira, ndio Rai mbali mbali zikatoka, watu wakasema wangelijua wangeliomba Serikali iwape Vijana Wapiganaji wa Jeshi JWTZ kazi yote kuanzia kuleta vifaa hadi zoezi Zima la kuandikisha na kuchukua taarifa za Vitambulisho vya Taifa, ni vile Vijana wa Jeshi ni wakakamavu wepesi na wachapa kazi!!!

    Hebu tazameni ile kuleta vijana wa JWTZ Maafande Wapiganaji wameleta kabla ya saa 12 asubuhi je kuandikisha si wangeanza na mapema sana?

    ReplyDelete
  4. Mdau wa 2 hapo juu,

    Ni sawa kwa kuwa suala la Congo-DRC ni suala la jirani zetu wakati suala la Malawi ni letu wenyewe hivyo tungeangalia Adui wa kupewa kipaumbele angalikuwa ni Malawi kwanza!!!

    Ziwa Nyasa mchezo?

    Kama tutalikosa ndugu zetu akina Kapteni Mstaafu John Komba watapata wapi kitoweo cha samaki, maji ya kunywa watapata wapi?

    Watasafiri vipi kutoka Kijiji hadi kijiji ukingoni mwa ziwa Nyasa? kwa kuwa ukishaingia ndani ya Boti ama usafiri wowote wa majini tayari unakuwa upo nje ya nchi ya Tanzania yaani upo Malawi!!!

    Mnaonaje uzito huo wa suala la Ziwa Nyasa?

    ReplyDelete
  5. Kama Maamuzi ya Mgogoro yataipa Malawi ushindi, itakuwa Tanzania ni nchi ya pekee dunia nzima kuwa na mpaka wa majini wa aina hiyo!

    Itakuwa ni ajabu na kweli na kubwa ya aina yake.

    Vigezo vipo vingi lakini kikubwa ni Sheria UN (Umoja wa Mataifa) ya Mipaka na kwenye maji ya mwaka 1982 inatupa nafasi labda ni kuwa suala litakuwa upimaji na kupewa Mpaka Kisheria ingawa tuliuweka kabla ya Sheria hiyo kuwepo.


    Wakati Sheria wanayodai Malawi ni ya Mkoloni ya mwaka 1890 ya Heligoland ambapo ktk Sheria Kimatifa inafahamika ya kuwa IKIINGIA SHERIA MPYA YA ZAMANI INAKUWA KAPUNI.!!!

    HIVYO SHERIA YA UN YA MWAKA 1982 ITAKUWA NA NGUVU KULIKO SHERIA YA MWAKA 1890.

    ReplyDelete
  6. NA KINGINE TUMESIFIA SANA JESHI LETU KWAMBA VIJANA NI WAKAKAMAVU NA WACHAPA KAZI SASA WANDUGU, HAWA VIJANA NI KWAMBA WANAZALIWA HUMU HUMU TENA WANAWAKE NDIO WENYE MAJUKUMU MAKUBWA KUONA KIJANA ANAKUA VIZURI, SASA ILE TABIA YA KUBAKA NA KUTUBAKA TUTOTO TUDOGO IKOMESHWE KABISHWA KWANI NDIO TAIFA LENYEWE, VITOTO VIKIENDELEA KUBAKWA SASA KUTAKUWA NA TAIFA GANI LA WATU GOI GOI, WATOTO NI TAIFA LA KESHO WALINDWE KWA GARMA YOYOTE ILE, NAWAKILISHA, FREEDOM OF SPEECH

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...