Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Watu na Makazi Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kupungua kwa mfumuko wa bei nchini kutokana na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma mbalimbali nchini. Kulia ni Meneja wa Idara ya Takwimu za Ajira na Bei.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO,Dar es salaam.

 Imeelezwa kuwa Tanzania inapiga hatua nzuri katika maendeleo ya uchumi kwa nchi za Afrika Mashariki kutokana  na  kupungua kwa mfumuko wa bei  wa taifa  hali inayoleta unafuu wa maisha kwa mlaji.

Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka 2013 kuanzia mwezi Januari mpaka mwezi Desemba umepungua hadi kufikia asilimia 7.9 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 16.0  iliyofikiwa mwaka katika mwaka 2012.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Franklin MzirayJanuary 09, 2014

    Sikukuu zimeisha na pote duniani watu wamerejea makazini. Hapa Mombasa raha zimeenda na msimu wake, tunachacharika na majukumu.

    Japo msimu wa sikukuu ulikuwa na jam iliyoshika sana hata magari zikishindwa kusonga, si ati lazima ilikuwa ati uende places za kujienjoy. Sasa jam ipo na lazima utoke hosii wende job, si ndio.

    Kama unataka kwenda Mumbai, au mji yeyote ile India, na huko utataka uwe unapeleka gari, basi kuja huku ujifunze.

    Madereva za hapa ni kama hawajuangi ishara zilizofungwa kwa gari. Bado wako wanatumia zile za mikono zaokuonyesha kama wanataka kupinda barabara. Tabu kwetu wahamiaji wa muda, ni pale ambapo utashindwa kuunderstand hiyo mkono ni signal au hiyo dereva anatupa jani la mirungi.

    Jam hapa lakini zinzkuanga mbaya kwa tuk tuk. Aii, hizi ni taaabu sana maana utapata kwa roundaboaut umesongwa na tuk tuk zaidi ya kumi pande moja na ile ingine mat mob hasa. Unajua zile vipanya za kwetu bado hapa zinatembea tao. alafu hao ni manderefa wenye wameenda skuli moja na wa huko tz.

    Sasa kama hizo si tabu, angalia vile wenye kwenda kwa miguu wanavyoruka barabara. Ni shida sana, barabara yote mnashare na wenye kwenda kwa miguu, wao wakikatiza na wewe ukienda mbele.

    Pamoja na kwamba hata watu wa middle class wakipeleka gari wanaacha madirisha wazi, wakivumilia joto kali la hapa coast, nawasifu kwa namna walivyosherekea sikukuu za end of the year.

    Utalii wa ndani hapa ndio pahala yake. Tangia before Christmas to new year, ukipita penye maduka au restaurant unapt ni group za watt sita, saba name na more, wakiwa ni family na extended family ambao wametoka bars kuja coast kujienjoy. Wanakula pamoja kwa restaurant na meza zinapangwa kwa six hadi zaidi. Akini sisi inabidi kukaa kaunta kukula.

    Nadhani ni muhimu kwetu, pamoja na kwenda mdenyi kuhesabiwa kila mwaka, tukaanza kujipanga kuvinjari katika maendeo yetu ya kitalii. Wale wa bara waje pwani, na wa pwani waende bara.

    watu wenye kipato cha kati wanatakiwa kukhakikisha kwamba wanapata quality time na jamaa zao kwa kusave kiasi kidogo cha pesa zao kwa ajili ya mwisho wa mwaka.

    Ila mhh, machungu ya Januari hata hapa yapo, na yamekuwa shubiri pale mabasi yalipokataliwa kusafiri usiku.

    Kwa ukumla hata hivyo, ni vyema kama jamii, tukawa tunaweka malengo yetu ya kiuchumi na ustawi wetu vyema ili tupate fursa za kujipumzisha ifikapo mwisho wa msimu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...