Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawatangazia abiria wote na wananchi kwa jumla  kuwa kutokana na kujaa maji eneo kati  ya stesheni za Godegode na Gulwe mkoani Dodoma na kuharibu tuta la reli,  unasikitika kutangaza kusitishwa kwa muda huduma ya usafiri wa abiria kuanzia leo Ijumaa Januari 10, 2014 hadi itakapotangazwa tena.
Wasafiri wote wenye tiketi halali wafike katika stesheni walizokatia tiketi hizo kwa ajili ya kurejeshewa fedha  kuanzia leo!
Aidha taarifa  hii iwafikie wadau wote wa usafiri na huduma ya reli ya kati na kwamba uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza..
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Paschal Mafikiri.
TRL Makao Makuu,
Dar es Salaam.
Januari 10, 2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Waliokwama njiani wasafirisheni kwa mabasi kama zamani

    ReplyDelete
  2. nani kakwama njiani? wa dodoma tulishasafirishwa tangu jana usiku, tushafika tuko majumbani.

    ReplyDelete
  3. Hii ni karne ya 21 -tujenge treni ya kwenda kasi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...