Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo.
Hiki ndicho ninachokifahamu mimi ndugu yenu.
Maisha ni vita, maisha ni mapambano na mtindo pekee wa kukusogeza mbele ni kupigana! Hata uwe mwema kiasi gani utakuwa na maadui, Yesu alikuwa nao, Mtume Muhammad alikuwa nao, Mandela alikuwa nao na hata Mahatma Gandhi alikuwa nao.
Hata ufanyeje maadui watakuwepo tu, utapingwa, utapuuzwa, hivyo basi kamwe usijaribu kuwafurahisha watu, eti unafanya vitu ili watu wakupende, utapoteza muda wako bure.
Kumbuka kuwafurahisha watu ndio barabara kuelekea kwenye umasikini, siku zote fanya kitu ambacho moyo wako unaridhishwa nacho. Watu watakucheka, watakutukana matusi yote lakini mwisho wa siku kama ukiendelea mbele hao ndio watakuja kukupa mkono wa hongera pale utakapoibuka mshindi.
USHUHUDA WANGU; Kwa miaka yote kumi na tano ambayo nimeishi na kufanya kazi Dar es Salaam, nimetukanwa sana, nimeitwa majina yote mabaya, nimehukumiwa sana. Badala ya kuwachukia walionitukana na wanaonitukana (hivi sasa wakisoma ) ambacho mimi hufanya ni kuziba masikio na kuyachukua matusi yao kama hamasa kisha kusonga mbele.
Najua wapo watakaolia pindi nitakapokufa, lakini pia wapo watakaofurahi na kufanya sherehe kwamba nimekufa, cha muhimu kwangu ni urithi nitakaouacha hapa duniani baada ya mimi kuondoka, si urithi wa mali bali idadi ya watu ambao Mungu atasikia sauti zao wakisema "Mtu yule alikuwa mwenye dhambi lakini alisaidia kutupa tumaini na maisha yetu yakabadilika." Hao wakiwa wengi itanitosha, yawezekana sauti zao zitamfanya Mungu aniangalie kwa jicho la huruma na kusema “KARIBU MWANANGU.”
Nawatakia mwaka mpya wenye mafanikio, kumbukeni katika nchi hii ukifanya kazi kwa nguvu na ukiwa na malengo nafasi ya kufanikiwa ipo bila kujali historia ya maisha yako.
NAMUOMBA MUNGU MWAKA HUU
UWE WA MPENYO KWA KILA MMOJA WETU.
Asanteni Mungu awabariki
Eric Shigongo James
Eric Shigongo James
Mkurungenzi Global Publishers Ltd


Ivi bwana michuzi hakuna kasehemu unaweza kuweka ka ku like meseji nzuri au ujumbe mzuri kama huu wa bwana Shigongo
ReplyDeleteKumbe busara kitu kigumu. Hayo kwamba kuna watu wakuchukia wanasubiri ufe hayakuwa ya lazima. Hata hivyo ingawaje sikufahamu nakutakia kheri jema njema na maisha marefu.
ReplyDeleteBro. Hakika umesema
ReplyDeleteMdau.jp
Well said.
ReplyDeleteAmen umenena vyema, ila naongeza uutafute kwanza uzima ule ujao. Kwani matendo yako wewe hapa duniani yatafuatana nawe peke yako kuurithi ufalme mbinguni ama kuangamia. Tajiri mmoja aliuliza nifanyeje niurithi ufalme wa mbinguni? Majibu. Uza uliyo navyo wape maskini na wahitaji kisha nifuate. Na dini safi isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni kwenda kuwatizama yatima na wajane katika dhiki yao na kujilinda na dunia pasipo mawaa. Ila utende mema, uwe tajiri kwa kutenda mema, na walio matajiri wa ulimwengu wasijivune, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha.
ReplyDeleteManeno mazuri..nimeupenda ujumbe wa bwana Eric..but kiukweli ndo dunia na maisha yalivyo.well said mr.Shigongo.Shukran.
ReplyDeletemdau wa UK
Erick umesema kweli. ni ujumbe wa matumaini kwa watu wengi waliokataa tamaa.erick tafuta nafasi uwafikie watu wengi.
ReplyDeleteNimependa sana ujumbe wa kaka yetu Erick "Kijana ambaye ni mfano kwa kila mpambanaji katika ardhi hii", ila napata pia wasiwasi wa baadhi ya sentensi zake k.m usifanye vitu ili kuwafurahisha watu, siku zote fanya vile vitu ambavyo moyo wako utaridhishwa navyo, lazima ukiri pia kuwa hapa uliweka pembeni chembechembe za utu sidhani km kila mtu angefanya anavyotaka ili kuupa moyo haki yake hii dunia ingekalika au kutawalika, hata hao uliowatumia kama mifano YESU, MTUME MUHAMMAD,MANDELA,MAHATMA GANDHI wameyafanya mengi kwa ajili ya watu si kwa ajili tu ya kufurahisha Mioyo yao moja kwa moja. Lakini pia uwepo wa maadui au wapinga maendeleo, dharau, chuki visimfanye mtu kuishi vile ambavyo tu anavyotaka bali kwa kufuata msingi na taratibu zilizopo za Mungu na kibinadamu tulizojiwekea.
ReplyDeleteKheri ya Mwaka Mpya.
Naitwa Edrew Kaduri nipo Uholanzi, katika jimbo la Friesland mji wa Drachten ni Mtanzania ninayeishi hapa kwa muda wa miaka mitano sasa.
ReplyDeleteKwanza nimpongeze ndugu yangu kama yangu Eric Shigongo kwa ujumbe huo lakini nina shaka kama kweli umetoka ndani ya uvungu wa moyo wake kutokana na sababu zifuatazo.
Ni kweli kuna ukweli ya hayo unayoyasema kwenye ujumbe wako lakini si bure kuchukiwa inawezekana una mambo ambayo unayafanya yanakuongezea maadui.
lakini kubwa kuliko yote ni kuwa mtu wa kupenda vita na malumbano kwa kuamini kuwa upo sawa katika kila jambo kitu kinachokufanya kujijengea maadui ndani na nje ya mazinmgira unayoishi.
Binafasi nakupongeza kwa uchapakazi wako ingawa kwa uchunguzi nilioufanya nimegundua kuwa una udhaifu mkubwa katika utendaji wako wa kazi kwani ndani ya maisha halisi ni tofauti na yale unayoyasema mbele ya umma.
umekuwa mfuasi mkubwa wa kutangaza ujasiramali na kuwawezesha watu wenye kipato kidogo na masikini lakini wafanyakazi wako wengi nawafahamu ni masikini wa kutupwa na wengi unawalipa mishahara midogo ndiyo chanzo cha wengi kukimbia baada ya muda mfupi.
Nadhani kama ukifanikiwa kurebisha ndani itakuwa ni rahisi kwako kuwapa wengine maisha bora kwani huku uholanzi upo msemo wa Kidachi usemao (eerste echte leven later) yaani maisha kwanza mali baadaye lakini wewe imekuwa tofauti na unayosema.
Kimsingi unafanya mambo ya kinafiki nafiki ili dunia ikuonee huruma lakini mimi nikiwa huku nimepata kujua mambo hayo kupitia kwa watu wako wa karibu, nakushauri badilika kwanza kisha uweze kueleza huruma na machozi (mededogen en tranen) kwa watanzania kwani hivi sasa kila kitu kiko wazi.
nakukubali kaka ila rekebisha hayo ikiwemo suala la kulipiza visasi ambalo umekuwa mfuasi mkubwa wa suala hili.
Mungu akubariki na kutia nguvu kwa wakati mwaka 2014.
Mimi ni mdau no. 1 wa Global Publishers kutoka hapa Drachten, Uholanzi.namba yangu ya simu ni +31 633 342 355