Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Kichina ya China Merchant Holdings International (CMHI) Ofisini kwake jijini Dar es salaam Januari 10, 2013. Kushoto kwake ni Kiongozi wa Ujumbe huo , Hu Jianhua na kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dr. Mary Nagu. Kampuni hiyo inatarajiwa kujenga bandari mpya ya Bagamoyo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Kiongozi wa Ujumbe kutoka Kampuni ya kichina ya China Merchant Holdings International (CMHI), Bw. Hu Jianhua kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu, jijini Dar es salaam Januari 10, 2014. Kampuni hiyo inatarajiwa kujenga kampuni mpya ya Bagamoyo. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. The mdudu,gooooood news but mbona hamna maelezo ya kutosha?

    ReplyDelete
  2. Hongera serikali at least kwa kutuonyesha kuwa huu mradi haukuwa another white elephant dream.kinachotakiwa sasa ni speed of action.unajua jirani zetu hawalali wakifanya makafara huu mradi wetu ufe....

    ReplyDelete
  3. Hapa ndio kiini cha Tanzania na Raisi Kikwete kutengwa ktk EAC!.

    Jamaa waliposikia Tanznia inampango wa kujenga Bandari ya Bagamoyo kwa gharama za US$ 11 Billion yenye uwezo wa kusafirisha Makontena 20 Milioni kwa mwaka, wakaanzisha 'Coalition of Willing' yaani CoW!

    Kuanzia kwenye Bandari, Reli zitatandikwa hadi Mwanza na Kigoma kwenda Congo-DRC na Burundi.

    Kazi kwao Rwanda na Uganda kuchagua kutumia Bandari ya mbali na Gharama za juu ya Mombasa ama Bagamoyo?

    Tupo kwenye Uchumi wa ushindani, sisi Bandari ndio hiyo inajengw huku Kenya na LAPSSET yao Bandari ya Lamu hadi Sudani Kusini Fedha hawajapata huku Juba kukiwaka moto kwa vita, ni wazi Mpango wa Lapsset Bandari ya Lamu utakuwa wa kiganjani, kazi kwao.

    Wataka Vikao vyao CoW lakini Tanzania mwendo mdundo, Tanzania haishikiki!

    ReplyDelete
  4. Good start for the government. Huu mradi ukianza tu naona wale mapacha watatu waliojitenga watatuheshimu sana. Wanatudharau kwa kile kinachoaminika kuwa ni nchi ya ubabaishaji. Sasa JK atawakomesha na hawatamsahau kwa bao atakalowapiga kufunga muhula wake uongozini.

    ReplyDelete
  5. Assalama Leko zako Jakaya Kikwete !

    Kikwete Shikamoo! hapo kwa kweli kazi umeifanya na kuinyanyua Tanzania kimasomaso.

    Alaaa kumbe ndio maana tunatengwa?

    Ni wazi Mradi huu ukikamilika na viongezeo vyake anavyosema Mdau wa 3 hapo juu Reli hadi Burundi na Congo DRC nadhani akina K-3 watakuja kumpa Shikamoo zake Jakaya Kikwete Ikulu Magogoni kama mimi nilivyotoa shikamoo zangu hapo!

    Ahhh!, acheni Jakaya Kikwete aitwe ''BALOZI DAKITARI'' maana ana Mipango yenye akili sana!

    ReplyDelete
  6. Rwanda, Uganda na Kenya HABARI NA SALAMU ZA MWAKA MPYA 2014 KUTOKA KWA KIWKETE NA TANZANIA NDIO HIZO!

    BANDARI MPYA YA BAGAMOYO KUBWA AFRIKA NZIMA NI NO. 1 INAJENGWA.

    SAFARI HII MTAZAA NA SISI TANZANIA NINYI NA HIYO COALITION OF WILLING YENU.

    KAZI KWENU!

    LITAWAKERA JIN MAX!

    ITAWAUMA SANA TAARIFA HII, KICHUNGU HUONJWA LAKINI MTAZOWEYA TU.

    ReplyDelete
  7. Mhe. Jakaya Kikwete inaaminika ndiye Raisi pekee ktk hii EAC ameumudu Muungano huu!

    Tazameni:

    1.Mwezi Mei-2013 anakuwa Raisi pekee duniani kuwashauri Kaguta M-7 na Kagame wakae na Wapinzani wao kupatana, Kagame anakasirika!

    2.Mwezi Novemba-2013 Jakaya Kikwete anatoa Hotuba kali anapasua jipu la Afrika ya Mashariki,,,eneo Zima linatikisika kuanzia Kigali, Kampala,Bujumbura na Nairobi inakuwa kama vile Raisi Kiwkete anaihutubia Afrika ya Mashariki!

    PANA HABARI ZA KUAMINIKA WAKENYA, WAGANDA NA WANYARWANDA HADI SASA NCHI ZA NJE NA NDANI WANGALI NA MACHAPISHO YA HOTUBA ILE WAKIRUDIA RUDIA KUISOMA!

    WENGI WAMEMKUBALI SANA JK NA KUWAKOSOA AKINA KAGAME, KENYATTA NA KAGUTA M-7 HASWA JUU YA SUALA LA UTENGANO KUITENGA TANZANIA NA PIA SUALA LA KUIPIGIA DEBE SUDANI YA KUSINI AMBAYO SIYO THABITI KISIASA NA USALAMA MBAYO TUNASHUHUDIA SASA IPO VITANI!


    Raisi Kikwete amekuja wakati Muafaka sana hasa juu ya Michakato mbali mbali ya hili dubwana la Afrika ya Mashariki.

    Ninatamani aendelee na Uongozi baada ya 2015 ili kuwabana hawa wakorofi ktk hii Afrika ya Mashariki ya mashaka mashaka ya akina Kagame, Kenyatta na Kaguta yenye Mipango mingi ya siri ya Kibindoni!!!

    ReplyDelete
  8. Tanzania DUME!

    Tanzania NYUNDO KUBWA!

    Tanzania NYUNDO YA CHUMA!

    Ni maajabu ya Musa CoW kuwa ni ngo'mbe wa Miguu Mitatu!

    ''Coalition of Willing'' ni ng'ombe mwenye miguu mitatu (Rwanda, Uganda na Kenya) mara zote ng'ombe wa namna hiyo atakuwa ni Jini na hatakuwa na umri mkubwa atakufa tu, kifo cha kimyakimya cha mapema mno kufuatia Miradi kama hii ya Bandari ya Bagamoyo!

    Kama 'CoW' angekuwa ni ng'ombe kamili mwenye Miguu minne yaani (Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi) na KICHWA TANZANIA angekuwa ni ng'ombe mwenye umri mrefu kimaisha!

    Hivyo watake wasitake Tanzania ktk EAC ndio kichwa!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...