JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 08 WOTE RAIA NA WAKAZI WA SANGE – BUKAVU NCHINI KONGO WAKIONGOZWA NA HESABU LUHIGITA (16) BAADA YA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI. 
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 12.02.2014 MAJIRA YA SAA 13:00HRS MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA IKUMBILO WILAYA YA ILEJE WAKIWA WANASAFIRISHWA KWENYE GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.136 AQC AINA YA FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA MUSSA DISI (35) NA MATEO KADUMA (30)  WOTE WAKAZI WA ISONGOLE AMBAO PIA WAMEKAMATWA PAMOJA NA GARI HILO. 
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KWA JESHI LA POLISI KUHUSIANA NA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI ILI HATUA ZA  KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
  
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...