Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiongea na Kamati ya Uongozi wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika jijini Dar es Salaam leo.
Mshauri kutoka UNESCO Dr. Daniel Ndagala akiwaelezea wajumbe juu ya Umuhimu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika jijini Dar es Salaam Leo. (Picha zote na Benjamin Sawe wa WHVUM)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Baada ya Ukombozi wa Bara la Afrika kutoka kwenye makucha ya Wakoloni adui mkubwa mbele ambaye Kamati inatakiwa kukabiliana naye ni:

    1.Umasikini uliokithiri Afrika,
    Bara linaongoza kwa idadi kubwa ya rasilimali kini wakazi wake wakiwa ni masikini wa kutupwa.

    2.Ujinga na Maradhi,
    Idadi kubwa ya Waafrika hadi leo wangali kwenye ujinga uliopindukia kiasi kwamba unachochea umasikini zaidi mfano kuamini sana Uchawi kama tulivyoona baada ya Loliondo-Tanzania watu kunywa vikombe na sasa shughuli ingalipo humu Afrika watu wakiwa wanakimbilia Nigeri kwenye Bwawa la ajabu.

    3.Mgawanyiko wa rasilimali usio sawa,
    Ni jambo la kusikitisha sana kuona 1% ya wakazi wa daraja la juu wa Afrika wakiwa wanamiliki rasilimali na Uchumi kwa 90% wakati asilimia 99% wakimiliki 10% ya rasilimali, Hivyo kwa URARI NA MLINGANOSHO HUU MGAWANYIKO WA MAISHA NI MKUBWA SANA HUKU KUNDI KUBWA LIKIWA MASIKINI.

    Kamati ya Urithi wa Ukombozi wa Mwafrika inatakiwa kuhamishia nguvu zake ktk Mtazamo wa haya matatu (3) hapo juu.

    ReplyDelete
  2. ok itakuwa vizuri hayo makumbusho ya uriyhi wa ukombozi wa mwafrica yakanyiwa hraka kuhifadhiwa mfano jengo alilofanyia harakati Samora Machel kule Bagamoyo halionyeshi kumbukumbu yoyote.Sijui ule mpango wa kujenga makao makuu ya ukombozi wa afrika kule bagamoyo umefikia wapi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...