Meneja Masoko wa Be forward Tanzania,Bwa Kohei Shibata (kulia) na Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Isaac Mbinile wakimkabidhi ufunguo wa gari mshindi wa gari aina ya Noah Marco Hingi (katikati) ambaye ni mwanafunzi wa kutoka hosipitali ya bungando, jijini mwanza.
Meneja Mkuu wa kampuni ya uagizaji na usambazaji magari ya Be forward Tanzania Issac Mbinile (kushoto) akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi gari aina ya noah mshindi (kulia). hafla hiyo ilifanyika leo makao makuu ya kampuni hiyo katika bustani za Palm Resdency , mkabala na hospitali ya saratani 'ocean road' jijini dar es salaam.
Kampuni ya uagizaji wa magari yaliyotumika kutoka JAPAN ya BEFORWARD imeendesha shindano la kuwapata washindi 25 duniani kote waliojielezea jinsi wanavyoweza kuitumia kampuni hiyo katika shughuli za maendeleo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook ambapo mtanzania MARCO HINGI ameibuka mshindi na kujishindia gari.
Akizungumza jijini DSM Afisa masoko wa kampuni hiyo KOHEI SHIBATA amesema shindano hilo liliendeshwa wakati wa sikukuu ya CHRISMASS ambapo wateja waliotembelea ukurasa wa facebook wa befoward walipata nafasi ya kuulizwa maswali na kujibu mambo kadha wa kadha
Kati ya washindi hao Tanzania imepata nafasi mbili ambapo mwanafunzi wa chuo cha afya cha BUGANDO MWANZA bwana MARCO HINGI ameibuka mshindi
Makabidhiano ya zawadi ya gari aina ya NOAH yenye thamani ya shilingi milioni 11.8 yamefanyika leo jijini DSM kati ya Afisa masoko wa kampuni hiyo KOHEI SHIBATA na Mshindi MARCO HINGI ambapo SHIBATA amesema hiyo ni moja ya mikakati yao ya kuongeza mauzo kwa kuwafanya wateja kuwa na imani nao kama anavyoeleza meneja mkuu ISAAC MBINILE
Kwa upande wake MARCO HINGI ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha afya BUGANDO mwanza amesema aliwaomba BEFORWARD kumpatia gari la kubebea wagonjwa kutokana na mradi wake alioubuni wa kusaidia mama wajawazito vijijini.
Aidha HINGI ameongeza kuwa baada ya kujibu swali la BEFORWARD walijitokeza watu wengi waliolipenda wazo lake kwa kuandika ‘like’ na hatimaye kuibuka mshindi.HINGI amesema atalitumia gari hilo kubebeea wagonjwa katika mradi huo waliouanzisha mkoani MWANZA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...