Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,Mh. Kaika Saning’o Telele akizungumza wakati akifungua warsha ya kimataifa inayojadili maswala ya Maendeleo, Miundombinu na Vituo vya maji,katika hoteli ya Bahari Beach,jijini Dar es Salaam.Warsha hiyo ya kimataifa ambayo inawakutanisha wanataaluma mbalimbali itafanyika kwa siku mbili huku mada nyingi zikitegemewa kuwasilishwa.Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji Eng. Bashir Mrindoko, anayefuatia aliyevaa miwani ni Katibu Mkuu Msaidizi Maendeleo ya Maji na Umwagiliaji nchini Malawi,Mama Erica Maganga, anayefuatia ni Mhandisi Mkuu Wizara ya Maji nchini Zimbabwe,Bi. Tatenda Mawokomatanda,na kulia kwa Naibu Waziri ni Afisa Taaluma kutoka UN yenye ofisi zake nchini Ujerumani,Dkt. Mathew Kurian.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji,Eng. Bashir Mrindoko (wa pili kulia) akifafanua jambo wakati wa mapumziko katika warsha ya kimataifa kuhusu maendeleo, miundo mbinu na vituo vya maji.kulia kwake anayesikiliza ni Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi,Mh. Kaika Saning’o Telele, anayefuatia kwa Naibu Waziri ni Mhandisi Mkuu Wizara ya Maji nchini Zimbabwe Bi. Tatenda Mawokomatanda, na Kushoto kwa Mrindoko ni Katibu Mkuu Msaidizi Maendeleo ya Maji na Umwagiliaji nchini Malawi,Mama Erica Maganga.
Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha ya kimataifa iliyofanyika katika hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach, Nchini Tanzania.Picha na Chris Mfinanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...