Mwana Diaspora Benja ambaye pia ni nyota katika kipindi cha kila wiki katika mtandao wa Vijimambo cha IJIWE CHA UGHAIBUNI ametua Dar es salaam wiki hii akiwa katika harakati za kusaka fursa ya uwekezani na kutoa ajira kwa ndugu, jamaa na marafiki. Hapa ni katika kiota cha Break Point ya mjini ambako leo ameandaa dina la mchana kwa wadau kadhaa akiwamo Ankal

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Kwa moyo alioonyesha ndugu Benja wa kuja moja kwa moja na sio kutuma Maombi ktk Blogu ya kutaka Pasipoti na Uraia wa Tanzania, napendekeza yeye apewe Uraia na Pasipoti haraka sana, kisha apewe Mipango ya Uwekezaji!

    Ninyi mnaoombea huko Majuu asiye kuja Bongo na lake halitakuwepo!!!

    ReplyDelete
  2. Dina la mchana?
    Benja kama wahenga wasemavyo iwe ni Mangaribi au Mashariki nyumbani ni nyumbani.

    ReplyDelete
  3. Dina inaweza kuwa muda wowote. Mdau hapo juu angalia kwenye kamusi ya Kiinglish. Maana ya dina kwa kiinglish ni "the main meal of the day".

    ReplyDelete
  4. Aja leo chungu kimesha wiva!Kilipokuwa kinaaandaliwa alikuwa wapi,kilipotokota jee alikuwa wapi.

    ReplyDelete
  5. Eti Ndug.Benja,ukirudi ughaibuni utawaambia nini wale waliondoka nchi hii(TZ) na kujiripua huko kwa kutumia majina ya kijipakiza?Vyeti vya kuzaliwa jina jengine,mikoba walioyonayo haikubaliani na majina ya vyeti vyao vya kuzaliwa TZ na sasa wanaurandia uraia pacha. Jee utawawasa nini?walie au wachekelee mess waliyoifanya? Kwani yawezekana mtu mmoja akawa na ID mbili chini ya majina mawili tafauti akiwa na sura moja?

    ReplyDelete
  6. Kadi ya chama unayo ?
    Ubunge unalipa vizuri tu.

    ReplyDelete
  7. Mdau#1,
    Kwanza, pasipoti zilitengenezwa sababu watu wanakaa na wanasafiri mataifa mengine, siyo Bongo pekee. Wabongo wote hawaishi Bongo.(tutumie bongo zetu kama jina letu jamani).
    Pili, siyo kila mtu alieko majuu(ambako siyo mbinguni)anauwezo wa kuwekeza, tajiri.Jamani majuu watu wanachakalika, na wengine maisha siyo mazuri.Nampa hongera ndugu Benja kwani kuwekeza Bongo nako kunaitji moyo sana.
    Tatu, wacheni kuaandika vitu visivyoeleweka ni unyanyasaji wa ndugu zenu. Ingawa wengi mnaona sifa kuandika lolote lakini kumbuka wivu, roho mbaya, fitina, na ujinga ndio vikwazo vya maendeleo kwa Tanzania.
    Mwisho, naomba kuuliza wadau. Je sasa kila jamaa wa kija Bongo au tukija kuwekeza inabidi tujitangaze kwenye vyombo vya habari ili kuaminiwa unafanya kitu cha maendeleo Bongo? Je wale wasiopenda makuu inakuwaje? Au ndiyo janja mpya ya hizi blogs kijipatia ulaji?

    ReplyDelete
  8. Ankal,kumbe KUCHACHAMAA kuna faida zake ehhh? Unasema kiranja Ben kaja kutafuta na kufanya feasibility study nini awekeze TZ. Hayo ni matunda ya wale wabongo wote waliochachamaa katika walipochangia mada juu ya uraia pacha chini ya suala jee madispora mmeleta nini la maana Tanzania? Nashkuru suala limewagusa ndio mana huyu kiranja wa "Vijambo" ameona aje ajioshe sijui kwa niaba yake binafsi au ni kwa niaba ya wengine.Hata hivyo mcheza kwao hutunzwa .Kama kweli ndugu Ben tafuta fursa ya kuwaneemesha wengi na Taifa kwa ujumla.Good luck !!

    ReplyDelete
  9. Ankal mtamfilisi babu wa watu kabla hajawekeza! na wewe Benja angalia wabongo wanapenda dezo!

    ReplyDelete
  10. Aahaaa ahaaaaa, Anonymous uliyesema, "Ankal mtamfilisi babu wa watu kabla hajawekeza! na wewe Benja angalia wabongo wanapenda dezo!" Sina mbavu. Umeona wabongo tunavyopenda vya kirahisi rahisi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...