
Na Andrew Chale
KAMPUNI ya uuzaji wa bidhaa za
majumbani na ofisini ya Home
Shopping Centre (HSC) imemzawadia
mshindi wake wa kwanza
wa ‘pendezesha nyumba na HSC’, Rehane Jaffer zawadi ya sh 500,000. Shindano hilo linaendeshwa
kwenye mtandao wa kijamii wa
Facebook kwa jina la
‘Give a Way’.
Mshindi alikabidhiwa hundi ya kiasi hicho cha pesa jijini
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki,
Meneja Mauzo na Masoko wa HSC,
Nadhir Mubarak Bahayan ambaye
aliwataka watanzania kushiriki
shindano hilo ambalo kila Ijumaa
watakuwa wakijishindia sh.
500,000.
“Wateja wetu wa HSC,
wanatakiwa kujiunga kwenye
mtandao wetu wa facebook na
kisha kututumia picha walizopamba
ndani ya nyumba zao zitokanazo
na bidhaa zetu,” alisema Nadhir.
Alisema shindano hilo litaendeshwa
kwa mwezi mzima wa
Machi 2014
.
Mshindi huyo aliipongeza
HSC kwa shindano hio na kusema
ni faraja kwake na familia yake.
Aidha zoezi hilo ambalo litaendeshwa
kwa muda wa mwezi mzima wa Machi
huku kila Ijumaa ikitarajiwa kutangaza
washindi na kukabidhiwa hundi
siku inayofuata.
Nadhir aliwataka wateja wao
kuwa na tabia ya kutembea kwenye
mtandao wa HSC, na kushiriki
kupitia https://www.facebook.com/hsctz
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...