Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akiwa na Makamu wake Jaji Augustino Ramadhani baada ya kuwasili bungeni mjini Dodoma na muda mfupi kabla ya kuanza  kuwasilisha rasimu ya Katiba Mpya. 
 Baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba  wakiwa wamesimama kupinga Jaji Joseph Warioba asiwasilishe rasimu ya katiba huku wakipiga kelele na kugomga meza.
 Baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba  wakiwa wamesimama kupinga Jaji Joseph Warioba asiwasilishe rasimu ya katiba 

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akijiandaa kuwasilisha rasimu ya Katiba Mpya. Hata hivyo zoezi hilo liliahirishwa hadi kesho wakati baadhi ya wajumbe waliposimama na kutaka  baadhi ya kanuni walizojiwekea zifuatwe, baada ya kuonekana hazikufuatwa. 
 Muafaka ulifikiwa baadaye na rasimu hiyo itawasilishwa kesho kwa Jaji Warioba kufanya hivyo kwa masaa manne badala ya moja ama mawili yaliyopendekezwa awali.  Habari kamili  zitawajia muda mfupi ujao...

Picha na Deusdedit Moshi 
wa Globu ya Jamii, Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Afya ya binaadamu hasa afya ya akili inaweza kuyumba wakati wowote ule.

    Afya haina mdhamana kwa kuwa unweza kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Bunge la Katiba na Mhe. Rais Kikwete ukiwa na afya njama lakini ukafika Bungeni Dodoma ukiwa Mtambo ama Chizi fresh.

    Nina wasiwasi kitendo walicho fanya Wajumbe wa Bunge la Katiba dhidi ya Mhe. Joseph Warioba jana huenda wameyumba ktk afya yao ya akili!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...