Taarifa ya Uhakika iliyotufikia hivi punde ndani ya Ofisi za Globu ya Jamii,inaeleza kuwa Kivuko cha Mv. Magogoni kinachovusha watu na mali zao kutoka Magogoni - Kigamboni jijini Dar es Salaam,kimepatwa na kwikwi jioni hii baada ya kukatika kwa sehemu ya mkono unaoshika mlango wa upande mmoja wa kuvushia magari na waenda kwa miguu.Utaratibu wa kutengeneza Kivuko hicho unafanywa hivi sasa na Mafundi wa Kivuko huku Abiria wakiwa wamesimama pembeni kusubiria utaratibu mwingine.
Sehemu ya Abiria waliokuwa kwenye kivuko hicho wakiwa wamesimama pembeni kusubiria Kivuko kingine.
Ya nini bure kutahamaki na kuhangaika?
ReplyDeleteAu ramani ya Jiji hamuijui si mngepitia Mbagala hadi Kongowe na kurudi Kigamboni?