Marehemu Juma Bhalo

Mfalme wa Taarab nchini Kenya ambaye pia amejijengea jina katika nchi za Afrika Mashariki, Mohamed Khamis
Juma Bhalo, amefariki dunia. Bhalo amefariki dunia usiku wa Jumamosi akiwa nyumbani kwake eneo la Mji wa Zamani Mombasa, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Juma Bhalo  alizaliwa 1942 huko  Shela katika wilaya ya Malindi. Mwaka1954, alijiunga na shule ya msingi ya Sir Ali bin Salim , wakati huohuo familia yake ilihakikisha anahudhuria Madrassa ili kupata elimu ya dini. 
Bhallo mwenyewe aliwahi kusema hamu yake ya kuimba ilimuanza katika wakati huu na sauti yake kuwa na mvuto kutoka kipindi hiki alipokuwa Madrassa Akiwa na miaka 9 tayari muda wake mwingi ulitumika kusikiliza santuri, na akili yake ilianza kupenda sana muziki. 
Hakumaliza elimu ya msingi kwa kuwa wazazi wake walishindwa kulipa ada ya shule. Mwaka 1957 alihamia Mombasa na kupata kazi Forodhani, akiwa Mombasa alianza kukutana na kushirikiana na wanamuziki wa Taarab wa Mombasa. 
Hakuipenda sana kazi ya Forodha hivyo 1959 akahamia Tanga kwa mjomba wake, na hapo akajiunga na kundi maarufu la Taarab wakati ule lililoitwa Young Noverty, hapa alipata ujuzi mkubwa wa muziki wa Taarab. 
Alirudi kwao Malindi kwa muda mfupi na hatimae kurudi tena Tanga 1962 na kujiunga na kundi la Young Stars Taarab. 
Mwaka 1966 alirudi Mombasa na kuanzisha kundi la Bhalo and Party, kundi ambalo amedumu nalo mpaka Mauti yake. Mwaka 2007 baada ya zaidi ya miaka 50 ya kuwemo katika muziki wa Taarab, Juma Bhalo ambaye wapenzi wake walimuita Profesa na hata Mfalme wa Taarab alitangaza kuacha kufanya maonyesho ya wazi ya Taarab, alitangaza hilo siku alipopiga katika harusi ya mwanae. 
Alistaafu kazi hiyo kwa maneno yafuatayo  "Waswahili wasema kiwate kitu kabla hakijakuata. Kwa hivyo kama mulivyo nishuhudiya usiku huu nlivyowatumbuiza ambavyo ni kama kawaida yangu basi leo hii usiku huu kabla hawajaja watu wakasema ahhhhh Bhalo ashazeeka hawezi tena kuimba kwa hivyo najiuzulu ningali bado niko fiti. Kwa hivyo siimbi tena hadharani kikazi. Nawashkuru kwa ushabik wenu na musijali Mungu akiniwezesha Kasseti mpya ntawatoleya".
 Taarab yake iliegemea sana muziki wa Kihindi na hivyo kuwa tofauti na taarab nyingine
MUNGU AMLAZE PEMA PROFESA 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Juma Bhalo Mungu akurehemu, tunakumbuka nyimbo zako enzi zetu kama vile 'pete imenitoka'

    Nyimbo zilikuwa na mahadhi ya kihindi lakini maneno fasaha ya kiswahili.

    ReplyDelete
  2. Ha kumbe alikuwa hai, hakuna aliyembuka hadi leo kafariki?

    ReplyDelete
  3. kifo cha juma bhalo kiwe darsa kwetu hamna atakayebaki dunia hii sote tutakufa na muhim maandalizi ya huko tuendako kwa sisi waislam tunatakiwa tufanye mema tuswali mm natoa wito kwa waislam wote tuswalini huko tuendako ni kuzito tusiishi kama tumejiumba wenyewe

    ReplyDelete
  4. Ahhhhhh umenigusa ndipo mdau hapo juu,kuhusu wimbo wa pete.Sijui ilimponyoka au aliidondosha wapi marehem lakini wimbo wenyewe nami wanigusa sana. Marehem Jomo Kenyatta kuna siku alimshushuwa sana Baloo kwa wimbo huo kwa madai kuwa anamuharibia watu wake wa Kenya kwa pete gani hiyo aliyokuwa akiitafuta siku nenda siku rudi? Ingawa alimwita muongo lakini ni kweli si kawaida pete ikikutoka kurudi tena katika chanda.

    ReplyDelete
  5. Ohooooo hata nami naguswa mno na wimbo wa pete.Yangu ilinitoweka katika mazingira ya kutatanisha. niliipenda sana ingawa haikuwa ya dhahabu,lulu wala si ya fedha,lakini ilikuwa na ya mti wa mpingo-nyeusi tititi lakini niliipenda hadi na kutokuwa nayo basi NI simazi hadi leo hasa pale niusikiapo wimbo wa Marehem Juma Bhaloo hupukutikwa na machozi mwa mwa mwah . Mungu amlaze mahali pema.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...