Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kulia) akipokea ufunguo
ikiwa ishara ya kukabidhiwa magari matano kutoka kwa Balozi wa Japan nchini, Masaki
Okada wakati wa tafrija fupi ya makabidhiano ya magari hayo kutoka Serikali ya
Japan kwa ajili ya kusaidia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika majukumu yake
ya kuzima moto na uokoaji nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika katika viwanja
vya Kituo cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kulia) na Balozi wa Japan
nchini, Masaki Okada wakikata utepe ikiwa ishara ya makabidhiano ya magari
matano yaliyotolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya kusaidia Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji nchini. Magari hayo yamekabidhiwa katika viwanja vya Kituo
cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akiikagua moja ya magari
matano yaliyotolewa na Serikali ya Japan kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Magari hayo matano yalitolewa na Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada wakati wa
tafrija fupi ya makabidhiano ya magari hayo yaliyofanyika katika viwanja vya
Kituo cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam. Picha na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akitoa hotuba fupi ya
kuishukuru Serikali ya Japan kwa kuisadia wizara yake kupitia Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji magari matano kwa ajili ya kazi ya kuzima moto na uokoaji nchini.
Kushoto ni Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada ambaye alikabidhi magari hayo
kwa niaba ya Serikali yake. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna
Jenerali Pius Makuru Nyambacha. makabidhiano ya magari hayo yaliyofanyika
katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali Pius Makuru Nyambacha akitoa
hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (katikati) ili aweze kuzungumza na baadaye kukabidhiwa
magari matano ya kuzima motona uokoaji. Magari hayo yametolewa na Serikali ya
Japan kupitia balozi wake nchini, Masaki Okada (kushoto) katika viwanja vya
Kituo cha Zimamoto Kanda ya
Taswira ya magari matano yaliyokabidhiwa na Balozi wa Japan, Masaki Okada kwa niaba ya
Serikali yake. Magari hayo matano yaliyotolewa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
yalipokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima
katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam. Picha
zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. PICHA ZOTE NA KITENGO
CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA
NDANI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...