Mhe. Rais Teodoro Nguema Mbasongo (katikati) wa Guinea ya Ikweta akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kamati ya Mabalozi wa ACP baada ya kuzungumza na Kamati ya Mabalozi. Mhe Rais Mbasongo amesisitiza umuhimu wa nchi za ACP kushirikiana kujenga uchumi na kufanya biashara.
Akimkaribisha Rais huyo kuzungumza na Kamati ya Mabalozi wa ACP Balozi wa Tanzania Ubelgiji na Mwenyekiti kamati Balozi Dr. Diodorus Kamala (wa pili kulia) amesema nchi za ACP zinapaswa kuhakikisha Mikataba ya Ubia wa Kibiashara (EPAs) kati ya Jumuiya ya Ulaya na ACP inakuwa mikataba itakayosaidia nchi za ACP kuimarisha mtangamano wa nchi za ACP, kuhahakisha mapinduzi ya viwanda yanapatikana na kuwezesha nchi za ACP zinapambana na nguvu za utandawazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...