Mhe. Omar Mjenga (shati la Mandela katikati), Balozi Mdogo wa Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Dubai, akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa jumuiya ya watanzania waishio UAE.
Kikao hicho kilichohudhuriwa kwa wingi na vijana wa Jumuiya kilijadili hatua za mwisho za maandalizi ya sherehe ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano zitakazofanyika Le Meridien Hotel, Dubai.
Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu na Mtukufu Ahmed Bin Saeed Al Maktoum, Rais wa Shirika la Ndege la Emirates na Mkuu wa Idara ya Anga ya Dubai, watakuwa wageni rasmi. Sherehe hizo zitafanyika tarehe Aprili 14, mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...