Mkuu wa wilaya ya Rombo kulia akimkabidhi mwanafunzi Happnes John wa shule ya sekondari motamburu moja ya vitabu vya sayansi vilivyo tolewa na Airtell katika mpango wa shule yetu kwa shule ya sekondari Motamburu iliyopo Rombo mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Rombo kulia akimkabidhi mwalimu mkuu(Abel Masuki kushoto) wa shule ya sekondari motamburu baadhi ya vitabu vya sayansi vilivyo tolewa na Airtell katika mpango wa shule yetu shuleni hapo
====== ====== =======
Shule ya Motamburu Moshi yapata msaada wa vitabu toka Airtel.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia Program yake ya shule yetu imeendelea na zoezi lake la kuinua kiwango cha ufaulu katika masomo ya sayansi ambapo imekabidhi vitabu vya ziada na kiada katika masomo ya sayansi kwa shule ya sekondari ya MOTAMBURU iliyopo Kata ya tarakea wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro.
Akizungumzia msaada huo Meneja biashara wa Airtel kanda ya kaskazini Brightone Majwala alisema" program ya shule yetu inayolenga kutoa vifaa vya kufundishia mashuleni ikiwemo vitabu vya kiada na ziada kwa upande wa masomo ya sayansi ambapo mpaka sasa wameweza kufikia shule 900 katika baadhi ya mikoa ya Tanzania bara na visiwani ".
"Tutaendelea kushirikiana na serikali chini ya wizara ya elimu katika kuhakikisha tunaboresha elimu mashuleni na kupunguza changamoto za upatikanaji wa vitabu katika shule nyingi nchini. sliongeza Majwala
Mkuu wa wilaya ya Rombo Elinasi Pallangyo ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi katika hafla fupi za makabidhiano hayo ,alipokea msaada wa vitabu na kuukabidhi kwa uongozi wa shule baada ya kukabidhiwa na meneja biashara wa Airtel kanda ya kaskazini ambapo amewashukuru airtel kwa msaada huo ambao amesema umekuja wakati muafaka huku akiwakumbusha wadau wengine kuiga mfano wa Airtell Katika kuchangia maswala muhimu ndani ya sekta ya elimu hususani katika maeneo ya vijijini.
Akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya shule kwa mkuu wa wilaya mkuu wa shule ya sekondari MOTAMBURU Abel Masuki ameishukuru airtel Tanzania kwa msaada huo ambao wamesema Airtel imeonyesha kuwa mfano mkubwa kwa makampuni mengi kwa kuungana na serikali kutekeleza sera ya elimu ya kuwaelimisha watanzania wengi hasa walio maskini kuwaondolea ujinga lakini pia akatoa changamoto ya vifaa vya maabara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...