Meneja Uwekezaji katika Jamii na Udhamini wa Benki ya NBC, Rukia
Mtingwa akifanyiwa uchunguzi wa afya ya kinywa na Dk. Asnath Katoto wa Metropolitan Health
Insurance, wakati wa maadhimisho ya wiki ya Afya ya benki hiyo ambayo
wafanyakazi wa benki hiyo walipimwa vipimo mbalimbali ili kujua hali
za afya zao na kupata ushauri. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
Mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya NBC, Leah Yusuf Mndolwa (kushoto)
akitolewa damu ili kupimwa afya yake na Mtaalam wa Maabara kutoka
Metropolitan Health Insurance, Scanderia Mambaya wakati wa maadhimisho
ya wiki ya Afya ya benki hiyo ambayo wafanyakazi wa benki hiyo
walipimwa vipimo mbalimbali ili kujua hali za afya zao na kupata
ushauri. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya NBC, Cecilia Machaku (kushoto) akifanyiwa uchunguzi wa afya yake katika zoezi hilo jijini Dar es Salaam. Anayempima ni Dk. Asnath Katoto wa Metropolitan Health
Insurance.
Mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya NBC, Leah Ntambula (kushoto) akipimwa
msukumo wa damu (BP) na Dk. Asnath Katoto wa Metropolitan Health
Insurance wakati wa maadhimisho ya wiki ya Afya ya benki hiyo ambayo
wafanyakazi wa benki hiyo walipimwa vipimo mbalimbali ili kujua hali
za afya zao na kupata ushauri.
Meneja wa Benki ya NBC, Tawi la Corporate, Godfrey Ndossa (kushoto) akipimwa
uzito na urefu ikiwa ni moja ya vipimo vya afya na Josephine Sempanga's wa Metropolitan Health
Insurance wakati wa maadhimisho ya wiki ya Afya ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kuna uhusiano kati ya uzito na urefu kwa mtu mwenye afya bora.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...