
Mwenzeshaji wa Mafunzo ya waandishi wa habari bwana Ndimata Tegambwage
akiongea wakati wa uzinduzi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
Tanzania imedhamini mafunzo ya wapigapicha yatakayofanyika kuanzia
kesho katika kituo cha Msimbazi jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana
na MP5 2011 Entertainment. Pichani katikati ni Afisa mawasiliano na
Matukio bi Dangio Kaniki akifatiwa na mratibu wa semina Mpochi
Selemani.
.jpg)
Hayo yalisemwa Jijini Dar es Salaam jana na Afisa Uhusiano na Matukio
wa Kampuni ya Airtel Dangio Kaniki alipokuwa akizungumza katika
ufunguzi wa mafunzo ya siku nne kwa wapiga picha wa habari kuwajengea
uwezo kufanya kazi katika mazingira hatarishi.
"Tutaendela kuwapatia mafunzo wapiga picha ili wapate ujuzi zaidi
katika utendaji wao wa kazi kwa kuwa mabalozi wetu,na tutawatafutia
vifaa vya kisasa kwa ajili ya kufanyia kazi katika mazingira
hatarishi"alisema Dangio
Mafunzo hayo yanaendeshwa na Baraza la Habari (MCT),na kudhaminiwa na
kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na kampuni ya MP5 2011
yanashirikisha wapiga picha kutoka magazeti na TV.
Akizungumza katika mafunzo hayo mshiriki Suleiman Mpochi ambae pia ni
mratibu wa mafunzo hayo alisema watanufaika nayo kwa kuwa watajifunza
mbinu mpya za kufanya kazi katika mazingira hatarishi pamoja na
kufuata maadili ya taaluma ya waandishi wa habari.
Kampuni hiyo ni mara ya tatu inadhamini mafunzo hayo kwa wapiga picha
za habari ambamo Mwezeshaji katika mafunzo hayo Mkongwe wa Habari
katika fani ya habari Ndimara Tegambwage aliiomba kampuni kuendela
kudhamini mafunzo hayo na kuwapatia zana za kisasa za kazi wapiga
picha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...