Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania na aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2001,Hapiness Millen Magese akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro,jijini Dar es Salaam Mei 28,2014 kuhusu kuanzishwa kwa Kampeni ya kuhamasisha wanawake na vijana kupaza sauti zao wanaposumbuliwa na ugonjwa wa ‘Endometriosis’ baada ya yeye kuathirika na Ugonjwa huo kwa kipindi kirefu.
Amesema wanawake wengi na wasichana wamekuwa wakisumbuliwa lakini hawajui kama ni tatizo kubwa linalohitaji utafiti mapema kwa ajili ya kutafuta suluhisho. 
 "Hili ni tatizo ambalo limenitesa tangu nikiwa na umiri wa miaka 13, na kuniathiri mpaka leo hii sina uwezo wa kupata mtoto kwa njia ya kawaida.  Ila nina nafasi ya kuweza kupata mtoto kwa njia mbadala, mfano kwa njia ya kupandikizwa, au kupandikiza kupitia mwanamke mwingine kwa kutumia mayai yangu, na njia ya tatu ni kuasili, alisema Magese kwa ujasiri wa hali ya juu. 
 Jumapili ya wiki hii  yeye na wataalamu watatoa mafunzo kwenye fukwe za Coco beach jijini Dar es salaam ambapo watu wataelimishwa athari na nini kifanyike ikiwa watagundulika kusumbuliwa na tatizo hilo.
Daktari bingwa wa masuala ya wanawake na uzazi ‘Endometriosis’ wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk. Belinda Balanda,  akielezea seli za mji wa uzazi zinazokuwa nje ya uzazi ambazo hushambulia eneo hilo na kumsababishia mwanamke maumivu makali wakati wa mzunguko wa hedhi.
Wadau kutoka sekta mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...