Na John Gagarini, Kibaha 
 JUMLA ya warembo wanane wanatarajiwa kuchuana kwenye shindano la kumtafuta mrembo wa wilaya ya Kibaha mkoani Pwani shindano linalotarajiwa kufanyika leo Mei 30 mwaka huu kwenye ukumbi wa Container Bar Maili Moja Kibaha. 
 Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha mratibu wa shindano hilo Teddy Chilala alisema kuwa maandalizi ya kufanyika shindano hilo yanaendelea vizuri na kinachosubiriwa ni siku ya shindano hilo. 
 Chilala alisema kuwa warembo hao nane walikuwa wakifanya mazoezi ya kujinoa na shindano hilo vilivyo katika ukumbi wa Blue Nile na kuwa maandalizi yote kwa ajili ya mchuano huo yamekamilika. 
 “Shindano letu tutalifanya kama ilivyopangwa na kwamba maandalizi yote yanaendelea vizuri kwani warembo wote wapo katika hali nzuri kwa ajili ya mchuano huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa sana kutokana na washiriki wote kuwa na vigezo vya kushinda,”alisema Chilala. Aidha alisema kuwa burudani mbali mbali za muziki zitatolewa ikiw ani pamoja na bendi ya JKT Ruvu chini ya kiongozi wao mpya Amigo Ras pamoja na Toto Tundu.
 “Shindano la mwaka huu litakuwa la aina yake kutokana na kuwashirikisha warembo ambao ni wazawa wa Wilaya ya Kibaha, hivyo ametoa wito kwa wakazi wa Kibaha na maeneo mengine ya jirani kujitokeza kwa wingi kwenda kushuhudia onyesho hilo,” alisema Chilala. 
 Aliwataja warembo hao kuwa ni Merry Samweli, Derice Kalinga, Rosana Msangi, Mary Mpelo, Agata Nelson, Oliva Chales, Arafa Shabani pamoja na Jennifer David.
 Aliongeza kuwa wadhamini katika shindano hilo ni JKT Ruvu, Silver Hair & Beauty Salon, Dar City College, Mtali Promotion, Michuzi Blog, Blue Peal Hall pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvester Koka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...