Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus
Mwamanga (aliyesimama)akitoa ufafanuzi
juu ya utekelezaji
wa Mpango wa Kunusuru
Kaya Masikini
kwa walengwa wa Mpango huo (hawapo pichani).
Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha mkoani Pwani Tatu Seleman (mwenye miwani) akiangalia moja ya mikeka iliyosukwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini,PSSN, katika kijiji cha Vikuge kama njia mojawapo ya kukuza kipato cha wananchi.
Walengwa wa Mpango wa kunusuru
kaya masikini
katika kijiji cha Vikuge wilaya ya Kibaha mkoani Pwani
wakiwa katika mkutano uliohudhuriwa pia na wajumbe wa kamati tendaji ya TASAF (hawapo pichani) iliyotembelea kijiji
hicho kukagua shughuli
za Mpango huo zinavyoendelea.
Karibu wageni hivi ndivyo anavyoelekea kusema Mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza(aliyeko mbele
ya wajumbe) wakati alipowakaribisha
wajumbe wa kamati tendaji ya TASAF iliyomtembelea
ofisini kwake kabla ya kutembelea vijiji
vya Vikuge na Misufini kukutana na walengwa wa Mpango wa kunusuru
kaya masikini ,PSSN.
Kaimu mwenyekiti wa kamati tendaji ya TASAF Abbas Kandoro (katikati) akisisitiza jambo mbele ya Mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza (aliyevaa kilemba)
wakati wajumbe wa kamati hiyo walipomtembelea
mkuu huyo wa mkoa wa Pwani ofisini kwake kabla ya kutembelea vijiji
vya Vikuge na
Misufini katika wilaya ya Kibaha kukaguwa shughuli za walengwa wa Mpango wa Kunusuru
kaya masikini unaoratibiwa na TASAF,kushoto kwa Kandoro ni Mkurugenzi Mtendaji
wa TASAF , Ladislaus
Mwamanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...