Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF kanda ya Mashariki Bw. Sayi Lulyalya akiwaeleza
waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam (hawapo pichani ) kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na
Mfuko huo ikiwemo kukusanya zaidi ya bilioni 115 hadi kufikia machi 2014 sawa na asilimia 94 ya
lengo .kushoto ni Kaimu Meneja Masoko wa Mfuko huo Bi Rehema Mkamba.
(Picha na Jojina Misama)
Frank Mvungi-Maelezo
Mfuko wa pensheni wa LAPF umefanikiwa kusajili wanachama 20,214 kufikia
mwezi machi 2014 wakati lengo lilikuwa wanachama 15,287 katika kipindi hicho.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Kanda ya Mashariki wa mfuko huo bw. Sayi
Lulyalya wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam
Lulyalya alisema ongezeko hilo ni matokeo ya kuwepo kwa utekelezaji wa sera
nzuri zenye kuwajali wanachama wa mfuko huo na jaamii kwa ujumla.
Alisema kuwa mfuko huo umepanga kuongeza wanachama wake hadi kufikia
122,595 kwa kuwa mwitikio wa wananchi kujiunga na mfuko huo umekuwa
chanya kwa kiasi kikubwa.
“Tumekuwa na wanachama kutoka sekta binafsi ambao nao wameonyesha
mwamko wa kujiunga na uchangiaji wa hiari katika mfuko wetu ikiwa ni sehemu
ya kujiwekea akiba “ alisema Lyalya
Katika kutoa elimu kwa umma kuhusu faida wanazopata wanachama
wa mfuko huo lyalya alisema wamekuwa wakitoa elimu kwa njia ya
redio,Televisheni,Magazeti na na Makongamano.
Naye Kaimu Meneja Masoko wa Mfuko huo Bi Rehema Mkamba alisema kuwa
Mfuko huo umekuwa ukichangia katika huduma za kijamii ambapo katika mwaka
wa fedha 2013/2014 shilingi milioni 200 zilitengwa kwa ajili ya shughuli za
kijamii katika sekta za afya,elimu na kusaidia watu wenye mahitaji maalum.
Katika makusanyo mfuko ulijiwekea malengo ya kukusanya shilingi bilioni 122.7
ambazo ni michango ya wanachama na malimbikizo,ambapo hadi kufikia mwezi
machi 2014 mfuko umeweza kukusanya bilioni 155.5 sawa na asilimia 94 ya
lengo kwa kipindi hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...